Skip to main content

Posts

Showing posts from June 25, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

HOW TANZANIA BECAME UN’S EXAMPLE FOR EMPOWERING DOMESTIC WORKERS

 By Prosper Makene  Tanzania has continued to build its standing on the international stage after being recognized as an example to follow in advancing the rights of women, including domestic workers, during commemorations of the United Nations International Day of Women in Diplomacy held in Geneva, Switzerland. The recognition was issued during the Human Rights Debate on Women’s Rights held on the sidelines of the 62nd Session of the United Nations Human Rights Council, which is taking place in Geneva from 15 June to 7 July 2026. The session has drawn diplomats, UN officials, and civil society representatives to review progress on global human rights commitments, with a dedicated focus this year on gender equality and the protection of vulnerable workers. Speaking on behalf of the Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights, Ms. Chidi King, Director of the Gender, Equality and Inclusion Unit at the International Labour Organization (ILO), commended Tanzani...

MAHERA AIBANA SERIKALI KUHUSU SHULE ZA SEKONDARI,TAMISEMI YATOA MWELEKEO

 Naibu Waziri wa Ofisi ya waziri Mkuu  TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, amesema Serikali itafanya tathmini ya kina kuhusu mahitaji ya ujenzi wa shule za sekondari katika vijiji vya Isaba (Buruma), Magunga (Mirwa) na Nyamsangura (Bwiregi), kufuatia ombi lililowasilishwa na Mbunge wa Butiama, Dkt. Charles Mahera. Dkt. Mahera ameibua hoja hiyo bungeni akieleza kuwa wananchi wa vijiji hivyo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa shule za sekondari, hali inayowalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.  Dkt. Mahera alitaka kujua ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule katika maeneo hayo ili kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto. Akijibu swali hilo, Dkt. Dugange amesema kuwa kwa mujibu wa sera na miongozo ya Serikali kuhusu elimu ya sekondari, ujenzi wa shule mpya huzingatia mahitaji ya kila kata.  Ameeleza kuwa pale ambapo kata ina idadi kubwa ya wanafunzi au mazingira yanayoonyesha uhitaji wa shule nyingine, Serikali in...

BALOZI WA TANZANIA AKUTANA NA RAIS WA MKUTANO MKUU WA UNESCO

  Paris, Ufaransa. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UNESCO, Mheshimiwa Saidi Othman Yakubu, amekutana na Mheshimiwa Khondker M. Talha, Rais wa Kikao cha 43 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO na Balozi wa Bangladesh nchini Ufaransa, kwa lengo la kujitambulisha kufuatia kuanza rasmi kwa majukumu yake katika UNESCO.   Katika mazungumzo yao, viongozi hao walibadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ajenda za UNESCO, hususan namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za elimu, sayansi, utamaduni na mawasiliano, pamoja na nafasi ya Tanzania katika kuendeleza malengo ya shirika hilo. Balozi Yakubu alitumia fursa hiyo kumwalika Mheshimiwa Talha kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yatakayofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO jijini Paris, akieleza kuwa Kiswahili kinaendelea kuwa daraja muhimu la kuimarisha amani, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Kwa upande wake, Mheshimiwa Tal...

MBIO ZA SHUKRANI KWA MLIPAKODI KUELEKEA TUZO ZA RAIS KWA MLIPA KODI BORA NA MIAKA 30 YA TRA KUFANYIKA JUNI 27 2026

 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawakaribisha walipakodi wote nchini kushiriki matembezi na mbio za Shukrani kwa Mlipakodi kuelekea Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi bora na Maadhimisho ya miaka 30 ya TRA   Karibuni walipakodi wote na watanzania kwa ujumla siku ya Traehe 27 Juni, 2026 kuanzia saa 12 Asubuhi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na maeneo mbalimbali kwa mikoa yote kwa nchi nzima. ‘Miaka 30 ya TRA, Kulipa kodi ni Uzalendo na Ushujaa kwa Maendeleo na kujitegemea kwa Taifa letu’’

MADIWANI TARIME WATOA TATHMINI YA ZIARA DODOMA

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime na Diwani wa Kata ya Nyamisangura, Tobias Elias Ghati, amesema ziara ya madiwani wa halmashauri hiyo jijini Dodoma imekuwa ya mafanikio makubwa, ikiwapa nafasi ya kujifunza kwa kina utendaji wa Bunge na taasisi mbalimbali za Serikali, pamoja na kujionea miradi ya maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, Tobias  amesema ziara hiyo ilikuwa sehemu ya kuimarisha uelewa wa viongozi wa serikali za mitaa kuhusu mfumo wa utawala na uwakilishi wa wananchi katika ngazi ya taifa. Amesema awali madiwani walikuwa na matarajio ya kushiriki shughuli za kuapishwa kwa Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, lakini kutokana na changamoto za kiuratibu hawakuweza kufanikisha. Hata hivyo, baadaye walipata mwaliko kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete, uliowawezesha kufanya ziara rasmi ya Bunge. Tobias amesema ziara hiyo imewapa fursa ya kipekee kushuhudia namna Bunge linavy...

TANZANIA,JICA KUPANUA USHIRIKIANO KWENYE UTAFITI WA MADINI MUHIMU NA KIMKAKATI

 ✅Zaidi ya Wataalamu 30 Wanufaika na mafunzo kupitia Mradi wa  Kizuna 📍 Dodoma Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA) zimekubaliana kupanua wigo wa ushirikiano kwa kubainisha maeneo ya kipaumbele yatakayofadhiliwa kupitia JICA kwa msaada wa Serikali ya Japan ikiwemo utafiti wa madini muhimu na mkakati. Hayo yamebainishwa Juni 25, 2026 jijini Dodoma katika kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya Sekta ya Madini nchini. Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amesema ushirikiano na taasisi hiyo ni wa muda mrefu ambao kupitia JICA zaidi ya wataalamu 30 wa Sekta ya Madini wamepatiwa mafunzo nchini Japan yaliyowajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara na taasisi zake na kueleza kwamba, ushirikiano huo utaendelea kuimarishwa kwa manufaa ya Tanzania na Japan. Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa JICA nchini Tanzania, Dkt. Kats...

KIJAJI: TUTACHUKUA HATUA ZA KISHERIA ATAKAYEBAINIKA KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI,

 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ametoa onyo kali kwa watu wanaovamia maeneo ya hifadhi nchini, akisisitiza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na uharibifu wa maliasili. Waziri Kijaji ameyasema hayo leo Juni 25, 2026 jijini Dodoma Katika Mkutano wa Mwaka wa Wahifadhi Wanyamapori, unaofanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Uhifadhi Endelevu kwa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Taifa katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.” Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kijaji amesema sekta ya uhifadhi inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa zinazohitaji ushirikiano wa wadau wote ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Amesema moja ya changamoto kubwa ni ongezeko la migongano kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu, hali inayosababisha uharibifu wa mashamba, makazi na mifugo, hususan katika maeneo ya vijijini. Ameeleza kuwa hali hiyo inachangiwa zaidi ...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA HOSPITALI KUU YA JWTZ MSALATO

 Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), tarehe 23 Juni 2026, ilifanya ziara katika Hospitali Kuu ya Kanda ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Msalato, jijini Dodoma, kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo.  Katika ziara hiyo, Kamati ya NUU ilipokelewa na uongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho. Ziara hiyo ni sehemu ya jukumu la Kamati la kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo chini ya sekta ya ulinzi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya inayolenga kuboresha huduma za matibabu kwa wanajeshi, familia zao na wananchi kwa ujumla.  Kamati hiyo, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Pascal Chinyele, ilitembelea maeneo mbalimbali ya hospitali na kujionea hatua za utekelezaji wa mradi huo wa kimkakati.  Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mheshimiwa Pascal Chinyele...

SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

 Na, Mwandishi Wetu – Dodoma SERIKALI imesema itaendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa maafa nchini ili kupunguza madhara yanayosababishwa na majanga mbalimbali ambayo yamekuwa yakigharimu maisha ya watu, kuharibu mali na kurudisha nyuma maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa hii leo 25 Juni, 2026 na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. James Kilabuko, wakati akifunga Jukwaa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa lililojadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kuzuia na Kukabiliana na Madhara ya El Niño Jijini Dodoma. Amesema Tanzania imeendelea kukabiliwa na matukio ya maafa yanayosababisha athari kubwa kwa wananchi na uchumi wa Taifa, hali inayolazimu kuwepo kwa maandalizi madhubuti ya kukabiliana na changamoto hizo kabla hazijatokea. “Nchi yetu imekuwa ikishuhudia matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa na kuathiri mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii. Majanga hayo yamesababisha vifo, ulemavu wa ku...