Na Shomari Binda-Musoma KASI ya ujenzi wa shule mpya za sekondari katika jimbo la Musoma Vijijini umezidi kushika kasi kubwa ili kuongeza idadi ya shule na kutoa fursa ya ukaribu wanafunzi kupata elimu. Kufuatia hilo wananchi wa Kata ya Etaro Kijiji cha Mmahare wameanza ujenzi wa msingi wa madarasa ya shule mpya ya sekondari ikiwa shule ya tatu kwenye Kata hiyo. Leo machi 10/ 2025 mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amekabidhi kamati ya ujenzi wa shule hiyo mifuko 50 ya saruji kati ya mifuko 155 aliyoahidi kuendelea na ujenzi na watakabidhiwa mingine kadri wanavyotumia. Hivi karibuni mbunge wa jimbo aligawa saruji mifuko 150 kwa kila kijiji kinachojenga sekondari mpya fedha za saruji hiyo ni zile za mfuko wa jimbo Profesa Muhongo wakati akikabidhi mifuko ya saruji Kijiji cha Mmahare Kata ya Etaro amekipongeza na kukipa hongera kwa kasi nzuri ya ujenzi na tayari kimetumia mifuko yote 150. " Nipongeze kasi kubwa ambayo inafanywa na wananchi wa Ki...
Marato tv - Sauti ya Jamii