Skip to main content

Posts

Showing posts from December 2, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Majaliwa Kumwakilisha Rais Samia Mkutano wa Majaji na Mahakimu Afrika Mashariki

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Disemba 03, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Ishirini na Moja wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Grand Melia, jijini Arusha.

Tanapa Yapokea Mitambo na Malori Yenye Thamani ya Shilingi Billioni 6.4

Na Philipo Hassan/ Dar es salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amewakabidhi TANAPA Malori matano na mitambo mitano yenye thamani ya Dola milioni 2.4 sawa na shilingi Bilioni 6.4 za Kitanzania, tukio hilo limefanyika leo Disemba 2, 2024 katika Ukumbi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Mpingo House) jijini Dar es salaam. Vifaa hivyo viliyonunuliwa kupitia mradi wa Dharura kwa Uhifadhi na Utalii Tanzania (Emergency Recovery Support for Biodiversity in Tanzania) kupitia benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW). Akizungumza katika makabidhiano haya Balozi Dkt. Chana alieleza kuwa vifaa hivyo vitaboresha shughuli za Uhifadhi pamoja na miundombinu katika Hifadhi za Taifa Serengeti na Nyerere kwa malengo ya kupunguza athari zilizosababishwa na janga la UVIKO-19 kwenye Utalii na Uhifadhi. Dkt. Chana alisema “Nawaagiza Bodi na Wakuu wa Mashirika ya TAN

Dkt. Biteko ataka Watafiti, Wabunifu Ndani na Nje ya Nchi Watambuliwe Kuleta Maendeleo

*📌 Azindua Kongamano la 9 Sayansi, Teknolojiana Ubunifu* *📌 Asema Watafiti waendelezwe, wasivunjwe moyo* *📌 Azindua Mfuko wa mikopo nafuu “SAMIA FUND”* *📌 Norway Yaahidi kuendelea kufadhili utafiti wenye tija*   *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema umefika wakati kwa Serikali na taasisi na Mashirika kutambua, kuthamini na kutumia tafiti za wanasayansi wa ndani ya nchi ili kutatua changamoto zilizopo. DKt. Biteko ameyasema hayo leo Disemba 2, 2024 wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na maonesho linaloendelea Jijini Dar es Salaam. Amesema wanasayansi nchini wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kutafuta suluhu ya matatizo mbalimbali katika jamii lakini kazi zao zinatambuliwa zaidi nje ya nchi kuliko zinavyotambuliwa nchini jambo ambalo linaweza kuwavunja moyo. “Kongamano hilo ni la kujad...

Waziri Kikwete akabidhi Tiketi Vijana Kwenda Nje ya Nchi Kwa Mafunzo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, leo amewakabidhi tiketi za safari kwa vijana 26 kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wanaokwenda kwenye programu ya mafunzo kwa vitendo nje ya nchi. Vijana hao watakwenda nchi za Ujerumani, Sweden, na Denmark,kupitia programu inayowezeshwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Ushirika wa Wajasiriamali Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUGECO)

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt Samia atoa Nishani kwa Majenerali,Maafisa na Askari wa Jwtz

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa JWTZ jijini Arusha tarehe 02 Disemba 2024. Nishani hizo ni pamoja na Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ. Aidha,Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Maafisa na Askari walioshiriki Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo. Akizungumza na Wanajeshi Kanda ya Arusha, Jenerali Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwatunuku Nishani hizo. Aidha, amewataka Wanajeshi kote Nchini Kuviishi Viapo Vyao walivyoapa, kufanya kazi kwa Nguvu zote kwa Uhodari, Uaminifu, Utii na Nidhamu ili kuweza kuilinda Nchi, kulinda Katiba na Kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Mameneja wa Tarura wa Mikoa na Wilaya Watakiwa Kufanya Ukaguzi na Matengenezo ya Miundombinu Mara kwa Mara

Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Mhandisi Victor Seff amewataka Mameneja wa TARURA wa Mikoa na Wilaya zote nchini kufanya ukaguzi na matengenezo  ya Miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na TARURA mara kwa mara ili kubaini kasoro na kuchukua hatua za haraka kuondoa kasoro hizo. Kauli hiyo ameitoa wakati alipofanya kikao kazi na Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa TARURA katika Ukumbi wa Odotorium, Millennium Tower - Makumbusho jijini Dar es Salaam Mhandisi Seff ameonesha kutofurahishwa na hali ya matengenezo ya Miundombinu ya Barabara zinazosimamiwa na TARURA kufuatia ziara yake ya hivi karibuni aliyoifanya katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani. " Suala la matengenezo ya Miundombinu ya Barabara bado hatujafanya vizuri sana. Ukiona maeneo mengi bado hayafanyiwi matengenezo kwa wakati na haswa upande wa madaraja na mifereji ambayo tukikutwa na mvua yanaweza kutokea majanga ikiwemo miundombinu ya barabara kukatika na hata kupelekea maeneo m...

Mbowe aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema

Kikao cha Kamati Kuu ya Chama kimeendelea leo tarehe 02 Desemba 2024 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe.