Na Shomari Binda-Musoma WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini( TARURA) na Wakala wa Barabara Nchini( TANROADS) mkoa wa Mara wameahidi kutoa kazi kwa vikundi vitakavyosajiliwa kwaajili ya kutunza na kuhudumia barabara. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TARURA mkoa wa Mara Mhandisi William Lameck alipokuwa akifunga mafunzo ya siku 14 kwa wanawake,vijana na makundi maalum watakao hudumia barabara. Amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa mkoa wa Mara katika kuhakikisha wanashirikiana kutunza na kulinda barabara. Meneja huyo wa TARURA mkoa wa Mara amesema serikali inatumia fedha nyingi kwaajili ya ujenzi wa barabara hivyo ni muhimu kuwa na matunzo shirikishi. Amesema serikali katika bajeti zake kwenye ujenzi wa barabara inawekwa asilimia 30 zaidi ya milioni 300 kwaajili ya vikundi vya kijamii vya kuhudumia barabara. Mhandisi William amesema watu 86 waliopata mafunzo hayo wanapaswa kuchangamkia fursa na kuanzisha vikundi kwa haraka ili waweze kupata kazi na kujipatia kip...
Marato tv - Sauti ya Jamii