Skip to main content

Posts

Showing posts from August 13, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Takukuru Mara Kushirikiana na Viongozi wa Dini Kutoa Elimu ya Rushwa Kipindi Cha Uchaguzi

Na Shomari Binda-Musoma VIONGOZI wa dini mkoa wa Mara kupitia kamati ya amani na maridhiano wamesema wapo tayari kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) kuelimisha Jamii kuhusu Rushwa hususani Katika Kipindi Cha uchaguzi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kikao kilichofanyika agosti 13 kwenye ofisi za Takukuru na kuwashirikisha viongozi wa dini,wazee na maafisa wa taasisi hiyo wamesema kikao hicho kimekuja wakati muafaka. Wamesema suala la rushwa linakatazwa hata kwenye vitabu vya dini na wao wapo tayari kuwahubiri waumini juu ya athari za Rushwa. Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Maridhiano ya viongozi wa dini mkoa wa Mara Jacob Rutubija ameishukuru Takukuru mkoa wa Mara,kwa kuwaona viongozi wa dini kuwa wanayo nafasi kubwa kwenye mapambano dhidi ya Rushwa. Shekh wa mkoa wa Mara ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo amesema viongozi wa dini wanao watu wengi na ujumbe watawafikishia juu ya athari kwenye uchaguzi. Kiongozi wa itifaki wa kamati ya amani na mar...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana na Kufanya Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  Agosti 13, 2024 amezungùmza na Makamu wa Rais wa Cuba, Mheshimiwa Salvador Valdes Mesa.  Mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole yamefanyika  Revolutionary Square, Havana.

Mhe. Hamad Masauni Atembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Comoro

Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro leo Agosti 13, 2024 umempokea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni. Mh Masauni ambaye amembelea Ubalozi huo kisha kupata nafasi ya kusalimiana na watumishi ubalozini hapo. Akiwa katika ubalozi huo waziri huyo wa mambo ya ndani ya nchi, amepokea pia taarifa ya kituo na masuala ya Watanzania waishio Comoro.  Mheshimiwa Waziri Masauni amepongeza juhudi zinazoendelezwa na Ubalozi katika kukuza mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Homa ya Nyani Yatangazwa Kuwa Dharura ya Kiafya Barani Afrika

Kituo cha Kudhibiti na Kujikinga na Majanga ya Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimeutangaza ugonjwa wa homa ya nyani (Mpox) kuwa janga la kimataifa. Kwenye taarifa yake, mkurugenzi wa Afrika CDC, Jean Kaseya amesema ugonjwa huo unasambaa kwa kasi miongoni mwa nchi za Afrika hivyo msaada wa jumuiya ya kimataifa unahitajika kwa haraka. Kwenye chapisho lake la Agosti 10 kwenye ukurasa wa mtandao wa X, Kaseya alisema Afrika ina chanjo 200,000 pekee huku mahitaji yakiwa chanjo milioni 10. Tangu kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwanzo mwaka huu zaidi ya watu 13,700 wameripotiwa kuambukizwa huku vifo vikifikia zaidi ya 450 kwenye Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo pekee. Virusi vya ugonjwa huo vimeripotiwa kusambaa kwenye nchi za Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kenye na Rwanda. Chanzo: bbc

Rais Mwinyi: SMZ Kujenga Barabara za Mijini na Vijijini

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia wananchi kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara mijini na vijijini, na imepanga hivi karibuni kujenga barabara ya kisasa kuanzia Tunguu hadi Makunduchi yenye urefu wa kilomita 43. Amesema barabara hiyo itakuwa na njia nne, taa, njia za wapita kwa miguu, mitaro ya maji, pamoja na bustani. Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 13 Agosti 2024, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu ya CCM za Tawi, Wadi, Jimbo, Wilaya, na Mkoa wa Magharibi kichama katika Ukumbi wa Mikutano, Viwanja vya Maonesho Nyamanzi, Dimani. Aidha, Dk. Mwinyi amesema kuwa uwepo wa vyama vingi ni kukuza demokrasia na siyo kuleta chuki na ubaguzi nchini, na amewataka wanasiasa kuhubiri amani na kunadi sera za maendeleo kwa wananchi. Vilevile, Dk. Mwinyi amewahimiza wanachama wa CCM kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la ...

Waziri wa Mamlaka ya Forodha wa China Awasili Nchini Kwa Ziara ya Kikazi

Waziri wa Mamlaka ya Forodha ya China, Mhe. Yu Jianhua amewasili nchini leo Agosti 13, 2024 kwa ziara ya kikazi ya Siku tatu. Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipokelewa na Naibu Katibu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa. Ziara ya Waziri Yu Jianhua inalenga kukamilisha makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini China mwezi Novemba 2022. Mhe. Waziri Yu Jianhua ndiye anahusika na kutoa vibali vya kufungua masoko ya bidhaa mbalimbali kuingia nchini China. Akiwa nchini Tanzania, Mhe. Yu Jianhua atakutana na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii; Wizara ya Kilimo; Wizara ya Uvuvi na Mifugo; Kamishna wa TRA; na atatembelea Bandari ya Dar es Salaam. Ujumbe wa Waziri huyo pia utatembelea Stesheni ya TAZARA ikiwa ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya Tanzania na China

Mhe. Katimba Awataka CHMT Halmashauri ya Chato Kujitathimini

Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amemtaka mganga mkuu na timu ya usimamizi wa shughuli za Afya wa Halmashauri(CHMT) ya Chato kujitathmini na kuhakikisha wanatoa huduma bora ya Afya kwa wananchi. Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo katika mji wa Chato mkoa wa Geita kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe.Mohamed Mchengerwa kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi - CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wilayani Chato mkoa wa Geita. Maelekezo hayo ya Mhe. Katimba ni kufuatia malalamiko yaliyoibuliwa na wananchi kuhusu mwenendo usioridhisha wa huduma za Afya. “Nitafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha kwamba mnatimiza wajibu wenu na DMO maelekezo uyapokee na nitafuatilia kwa karibu kuona utekelezaji na tunataka wananchi wa Chato wapate huduma ya Afyayenye ubora kwasababu mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya” Amesema Mhe. Katimba