Skip to main content

Posts

Showing posts from January 31, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia aungana na Wakuu wa Nchi za Sadc Katika Mkutano wa Dharura Nchini Zimbabwe

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe tarehe 31 Januari, 2025. Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na  baadhi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kabla ya kuanza kwa Mkutano wao wa  Dharura uliofanyika katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe tarehe 31 Januari, 2025.  Matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wak...

Ccm Kimbilio La Wananchi, Tujadili Mambo Yanayowahusu - Wasira

Na Mwandishi Wetu, Bunda MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema Chama ni kimbilio la wananchi hivyo lazima kijadili na kubeba shida za watu. Ameagiza vikao vya Chama vizungumzie mambo yanayowahusu wananchi kwa lengo la kusikia changamoto zao na kuwa sehemu ya kupatiwa ufumbuzi. Wasira alieleza hayo mjini Bunda leo Januari 31, 2025 alipokutana na kuzungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara. Amesisitiza kuwa siyo sahihi vikao hivyo kujadili mambo yasiyo na maana wakati wananchi kjatika maeneo husika wanakabiliwa na changamoto ambazo endapo zitasikilizwa na kufikishwa mbele ya mamlaka husika zitapatiwa ufumbuzi. “CCM ni lazima isikilize watu wanataka nini, sisi ni Chama cha watu na kwa kweli tunataka kiwe cha watu kwelikweli, vikao vyetu vya CCM vizungumze mambo ya watu, kama ni mambo ya wafanyabiashara wadogowadogo (machinga) tuzungumze kuhusu hilo, kama wana matatizo wakimbilie CCM kwa sababu wanajua huko n...