Skip to main content

Posts

Showing posts from March 30, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Kumwakilisha Rais Samia Mazishi ya Lukuvi

 Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba leo Machi 31, 2026 amewasili Iringa Mjini akiwa njiani kwenda Idodi kumuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. William Lukuvi. Kwenye uwanja wa Ndege wa Iringa, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James.

Wanu Akabidhi Vifaa Vya Tehama Vya Mamilioni Kwa Shule za Msingi na Sekondari

 SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, imetoa vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya jumla ya Sh. 769,390,000 kwa shule za msingi na sekondari 19 zilizopo katika mikoa tisa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Vifaa hivyo vinajumuisha madarasa janja, mbao janja, vishikwambi na kompyuta, ambavyo vinatarajiwa kuwezesha ujifunzaji kwa wanafunzi, hususan katika masomo ya sayansi na teknolojia. Aidha, walimu watanufaika kwa kutumia mbinu bunifu za ufundishaji pamoja na mifumo ya kidijitali kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kwa ufanisi zaidi. Hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo imefanyika leo Machi 30, 2026 jijini Dodoma, ambapo Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. *Wanu Hafidh Ameir*, alisisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuendeleza mageuzi makubwa katika sekta ya elimu kupitia matumizi ya teknolojia za kidijitali. Amesema mageuzi hayo yanalenga kuboresha elimu kwa kuimarisha elimu ya lazima ya miaka 10, kuendeleza mkondo wa elimu ya amali, na kuimarisha...

Rais Samia Aagiza Uwazi Manunuzi ya Umma, Asisitiza Uwajibikaji

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuimarishwa kwa uwazi na uwajibikaji katika manunuzi ya umma, akielekeza taasisi zinazokiuka taratibu kutajwa hadharani na kuchukuliwa hatua. Akizungumza tarehe 30 Machi, 2026, Ikulu Dar es Salaam, wakati wa kupokea Taarifa ya Mwaka ya Tathmini ya Utendaji wa Ununuzi wa Umma, Rais Samia amesema sehemu kubwa ya fedha za Serikali hutumika katika manunuzi ya umma, hivyo usimamizi madhubuti ni muhimu kulinda rasilimali za wananchi. “Ripoti zijazo zitaje wazi taasisi zinazofanya vibaya na zinazofanya vizuri, ili kuongeza uwajibikaji na kuchukua hatua stahiki,” amesema Rais Samia. Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kuhakikisha rasilimali za Serikali zinatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.

Mwili wa Lukuvi Kuzikwa Leo Machi 31 Katika Kijiji Cha Idodi Mkoani Iringa

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu Mhe. William Lukuvi, wafikishwa Kijijini kwao Idodi mkoani Iringa.  Mwili wa Mhe. Lukuvi ulisafirishwa kutokea Iringa mjini mara baada ya kufanyiwa Ibada Maalum na kuagwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kanisa Kuu - Kihesa, Jimbo Katoliki Iringa leo Machi 30, 2026. Mhe. Lukuvi alifariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa Leo Machi 31, 2026 Kijiji Idodi.

Millioni Nane za Aweso zasomesha Vijana 80 wa Hamasa VETA

Na: Mwandishi Wetu, Pangani Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani mkoani Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumaa Aweso, ameacha alama katika maisha ya vijana 80 wa Hamasa na Itifaki wa CCM wa wilayani Pangani baada ya kugharamia ada ya masomo yao kwa kulipa shilingi 8,220,000 kwa mwaka wa kwanza wa masomo yao ili kusoma kozi mbalimbali za ufundi katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha wilayani Pangani. Akikabidhi fedha hizo kwa niaba ya Aweso, Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Pangani, Nasri Mkalipa, amesema Aweso ameguswa na vijana hao ambao wanajitolea kufanya shughuli mbalimbali za Chama kwa moyo wa uzalendo, hivyo ameamua kusaidia kutimiza ndoto zao za maisha kwa kugharamia ada ya mafunzo yao VETA. "Mbunge wetu Jumaa Aweso ana upendo sana na vijana, kwa muda mrefu vijana wa Hamasa na Itifaki wamejitolea kufanya kazi za Chama bila malipo, hivyo katika kutambua mchango wao, Mbunge ametoa Milioni Nane Laki Mbili na Elfu Ishirini ili zilip...

Eng. Samamba Calls for Stronger Safety Management in The Mining Sector

📍Mwanza The Permanent Secretary in the Ministry of Minerals, Engineer Yahya Samamba, has directed officials of the Mining Commission, particularly Resident Mines Officers across the country, to strengthen safety and environmental supervision in mining operations through regular inspections, especially during the ongoing rainy season, in order to prevent accidents that may lead to serious injuries or loss of life. Engineer Samamba issued the directive while officiating at the opening of the Second Workers’ Council Meeting of the Mining Commission held in Mwanza City. The meeting brought together key stakeholders including the Chairperson of the Mining Commission, Dr. Janet Lekashingo, the Executive Secretary of the Commission, Engineer Ramadhani Lwamo, officials from the Ministry of Minerals, the Office of the Labour Commissioner, representatives from the Tanzania Government and Health Employees Union (TUGHE), as well as directors, managers and Resident Mines Officers from various regi...