Skip to main content

Posts

Showing posts from July 14, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Alipongeza Kanisa la TAG Kwa Kukuza Watoto Kiimani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelipongeza Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa mkakati wake wa kukuza watoto kiimani huku wakilijua na kulishika neno la Mungu.  “Pamoja na shughuli ya uinjilishaji, leo nimeshuhudia watoto wadogo wakisema maneno ya Mungu bila kusoma mahali popote na mwingine akiielezea Misingi ya Kanisa la TAG bila kusoma popote. Hii ni kazi kubwa, mnasathili pongezi.”  Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 14, 2024) wakati akizungumza na viongozi na waumini wa Kanisa la TAG ambako alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 85 yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Amesema kanisa hilo linawafanya watu kuwa wamoja, kuwa na uhusiano wa kiimani na kijamii na kutoa mafundisho ya umuhimu wa kushiriki katika huduma kutoa misaada, elimu, huduma za afya na maendeleo ya jamii. “Kanisa hili ni mfano katika kukuza umoja na ushirikiano kati ya Wakristo wa madhehebu mbalimbali na waamini wa dini nyingine nchini, kiten...

Elimu: Fahamu Muongozo wa Tcra Kwa Wasimamizi wa Makundi ya Mitandao ya Kijamii

Na Emmanuel Chibasa Mitandao ya kijamii kama Whatsapp, Facebook na Instagram imerahisisha mawasiliano kwa watumiaji kupata na kusambaza habari na kuwepo kwenye makundi mbalimbali. Katika matumizi ya mitandao ya kijamii watumiaji huwa wanaunganishwa katika makundi mbalimbali na wasimamizi wa makundi hayo. Kwa mujibu wa Muongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za Mawasiliano uliotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano wa mwaka 2019, Mtumiaji anapokua msimamizi wa kundi katika mitandao ya kijamii anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo. 1.Hakikisha unapata idhini ya mtumiaji kabla ya kumuunganisha kwenye kundi katika mtandao wa kijamii na kwamba anafahamu madhumuni na masharti ya kuzingatiwa anapojiunga na kundi unaloliratibu. 2.Hakikisha kama msimamizi wa watu walioko kwenye kundi lako, wanaelewa na kuzingatia na kujihadhari kuweka maudhui yasiyofaa kwenye kundi kwa mfano matusi, uchochezi, uzushi, n.k 3. Hakikisha watu waliopo kwenye kundi wanaelewa kwamba wana uhuru wa kutoka kwenye kundi ma...