▪️Waziri Mavunde aelekeza mchakato wa mabadiliko ya sheria kuanza. ▪️Aelekeza kanuni kubadilishwa kupunguza tozo kwa hekta kufikia 20,000. ▪️Wazalishaji Chumvi wampongeza Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa ujenzi wa kiwanda cha Chumvi Mkoani Lindi ▪️Serikali kuwezesha wazalishaji chumvi kumiliki viwanda vya kuchakata chumvi *Dodoma* Serikali ipo mbioni kutambulisha Leseni mpya ya uzalishaji wa chumvi ili kuiondoa chumvi katika kundi la madini mengine na hivyo kuchochea ukuaji wa tasnia ya uzalishaji chumvi nchini Tanzania. Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde na Uongozi wa Chama cha Wazalisha Chumvi Tanzania(TASPA),kikao ambacho kimelenga kuboresha sekta ya madini kupitia tasnia ya chumvi. “ Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan ametupa maelekezo mahsusi kuwezesha wachimbaji wa madini na wazalishaji wa madini chumvi nchini ili kuchochea ukuaji wa sekta ya madini. Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu cha uwepo wa Leseni moja ya uzali...
Marato tv - Sauti ya Jamii