Arusha NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila ameagiza wakandarasi wanaojenga barabara za Engosheraton, Olasiti na Oljoro patakapojengwa stendi mpya ya mabasi kwa Jiji la Arusha zikamilike kwa wakati. Agizo hilo lilitolewa Jijini hapa na Mhandisi Mativila wakati alipotembelea barabara hizo tatu zenye urefu wa kilomita 12.1 kupitia Mradi wa Kuboresha Miji (TACTIC) uliopo chini ya TARURA. Alisema barabara hizo tatu za Engosheraton, Olasiti na Oljoro zenye thamani ya shilingi bilioni 15.4 zinajengwa kwa kiwango cha lami lakini bado ukamilishwaji wake upo nje ya muda. Akizungumza mara baada ya kutembelea barabara hizo Mhandisi Mativila alisema ziara hiyo ni ya kawaida katika kuangalia maendeleo ya kazi zinazofanywa katika ujenzi wa barabara hizo. “Ujenzi wa barabara ya Oljoro bado upo nyuma kwa asilimia 35 kutokana na kubadilishwa kwa mchoro(dizaini) kutokana na kiwango chake cha usanifu na kuwa barabara ya Mkoa kutokana na ujenzi...
Marato tv - Sauti ya Jamii