Na Angela Sebastian; Bukoba Mwenyekiti wa umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kagera (UVCCM) Faris Buruhani amewaongoza wanafunzi 650 wa shule ya sekondari ya wasichana ya Omumwani iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani humo kupanda miti 2,000 kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassani. Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Faris alisema kuwa lengo la tukio hilo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika kulinda na kutunza mazingira, akisisitiza kuwa upandaji wa miti ni sehemu muhimu ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Alisema kuwa jumuiya hiyo imeamua kuonyesha uzalendo wa vitendo kwa kushiriki katika shughuli zenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla ambapo wanafunzi wasichanawa shule hiyo wamekuwa sehemu ya kumbukumbu katika sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa mwaka 2026 Alisema kuwa vijana wa mkoa wa Kagera wanamuunga mkono Rais na wanampongeza kwa kazi nyingi anazofanga ikiwemo kudu...
Marato tv - Sauti ya Jamii