Skip to main content

Posts

Showing posts from July 27, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Ashiriki Mbio za Hisani za Benki ya NBC

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 28, 2024 ameshiriki katika mbio za hisani za Benki ya NBC zilizoanzia na kuishia katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri jijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza benki hiyo kwa kaundaa mbio hizo zenye lengo la kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake Pia mbio hizo zimelenga kuchangia ujenzi wa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ridhiwani Kikwete Ashiriki Kikao Cha Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi Chalinze

Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhwani  Kikwete ameshiriki kikao cha madiwani wa Chama Cha Mapinduzi ili kuchagua diwani atakayegombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze. Mh Kikwete ambaye ni waziri ofisi ya waziri mkuu,anayeshughulikia kazi,Ajira na watu wenye Ulemavu,ameshiriki kikao hicho ambacho kimefanyika  Julai 26-2024 na kumchagua Bw Ramadhan Mawazo Mkufya kuwa mgombea kupitia chama cha Mapinduzi. Bw Mkufya anbaye ni diwani wa Kata ya Kibindu,amepata kura 18 kati ya 19 zilizopigwa.

Takwimu za Watu Waliotembelea Website ya Georgemaratotv Hadi 27 Julai 2024

Takwimu za watu waliotembelea website ya www.georgemaratotv inazidi kuongezeka. Kwa mujibu wa ripoti ya Wiki iliyotolewa 22 Julai 2024 Jumla ya watu waliotembelea walikua ni 5164  na Idadi ya watu Waliotembelea hadi 27 Julai 2024 ni 12423. Kwa upande wa viewers wiki ya 22 Julai 2024 walikua ni viewers 3.41K na takwimu za hadi kufikia 27 Julai 2024 Idadi imefikia 6.84K Tunapenda kukushukuru kwa kuendelea kufuatilia habari na matukio Mbalimbali  Kupitia. www.georgemaratotv.com Twitter: georgemaratotv YouTube: georgemaratotv

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...

Rais Dkt.Samia Ashiriki Mahafali ya Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi NDC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mahafali ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kozi  ya 12 kwa Mwaka 2023/2024, Kunduchi Jijini Dar es Salaam, leo tarehehe 27 Julia,2024. Baadhi ya Waambata Jeshi pamoja na Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kozi ya 12 kwa mwaka 2023/2024 wakiwa wamesimama wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa wakati wa kwenye Mahafali ya Chuo hicho Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Julai, 2024.