Skip to main content

Posts

Showing posts from August 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Tulia Aanza Kuomba Kura ya Ndiyo Jimbo la Uyole

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini anayemaliza muda wake na mtia nia wa Ubunge wa Jimbo jipya la Uyole kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 2 Agosti 2025, amejitambulisha rasmi kwa Wajumbe wa Mikutano ya Kata mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea uchaguzi wa ndani wa CCM unaotarajiwa kufanyika Jumatatu, tarehe 4 Agosti 2025, nchi nzima.  Katika mikutano hiyo, Mhe. Dkt. Tulia amewaomba Wajumbe hao kumpigia kura nyingi za ndiyo ili kupata ridhaa ya kuwawakilisha na kuwatumikia wananchi kupitia nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Uyole. Amewaeleza dhamira yake ya kuendeleza jitihada za maendeleo na kuhakikisha jimbo hilo linapata uwakilishi wenye tija na ufanisi. Kata alizotembelea ni pamoja na Mwakibete, Ilomba, Ilemi, Isyesye, na Itezi, ambapo aliwasilisha vipaumbele vyake vya maendeleo ikiwemo kuboresha huduma za elimu, afya, miundombinu na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Ufunguzi Michuano ya Chan 2024

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 02, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa michuano ya CHAN 2024, katika Dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.  Katika mchezo wa ufunguzi Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inachuana na Burkina Faso. Michuano hiyo inafanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda

Waandishi wa Habari Wahimizwa Kuhamasisha Ushiriki wa Wananchi Kupiga Kura

Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kuhamasisha na kuelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo tarehe 29 Oktoba, 2025. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu, uliofanyika tarehe 2 Agosti, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Mhe. Jaji Mwambegele amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu kwa kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu masuala mbalimbali ya uchaguzi. Ameeleza kuwa waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kutumia taaluma yao kuwaelimisha wananchi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ili waweze kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amewaku...

Dkt. Biteko Aomba Kura ya Ndiyo Kwa Wajumbe Bukombe

Mbunge wa Jimbo la Bukombe anayemaliza muda wake, Dkt. Doto Mashaka Biteko ambaye ameomba tena ridhaa ya kutetea kiti hicho, ameeleza furaha na shukrani aliyonayo kwa Wananchi wa Bukombe kufuatia ushirikiano waliompa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. @biteko Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 2, 2025 kwa nyakati tofauti wakati akiomba kura kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi wa Kata za Lyambamgongo, Uyovu, Bugelenga, Katome, Igulwa na Runzewe Mashariki zilizopo katika Jimbo la Bukombe. " Mimi na viongozi wenzangu wakiwemo wa vijiji na madiwani  ukianzia sekta ya Nishati tumesambaza umeme kila mahali, Sekta ya miundombinu tumeongeza mtandao wa barabara kutoka km 259 hadi km 1,445 na Sekta ya Elimu tunaongoza kwa kuwa na shule nyingi za Msingi na Sekondari tofauti na ilivyokuwa Mwaka 2015 hatukuwa na shule ya sekondari ya upili hata moja lakini mwaka 2025 tunazo shule TANO,  Kwa upande wa sekta ya afya tumepata miradi mbalimbali na fedha nyingi za kuboresha huduma za afya k...

Wizara ya Nishati na Taasisi zake zashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Dodoma

Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake zinashiriki Katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo  ambayo  yameanza Tarehe 1  Agosti Katika Viwanja Nzuguni Jijini Dodoma. Maonesho hayo yamebebwa na kaulimbiu iya " Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025",  Katika maonesho hayo ambayo yamefunguliwa na   Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor  Mpango, Watalaam wa Wizara pamoja na kueleza mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Nishati ikiwemo ukamilishaji wa Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere na Usambazaji wa Umeme Vijijini, wanatoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia   Aidha wananchi wanafahamishwa kuhusu mipango mbalimbali ambayo Wizara imepanga kutekeleza katika mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kusambaza umeme vitongojini na utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia. Taasisi za Wizara ya Nishati zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa M...

Maambukizi ya Njia ya Mkojo Yanavyowatesa Wengi Nchini

*Sababu,tahadhari na changamoto ya usugu wa dawa* *Na Mwandishi wa Makala za Moto* Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) yameendelea kuwa changamoto kubwa ya kiafya kwa watu wazima, hususan wanawake, lakini pia wanaume kwa kiwango kidogo.  Maelfu ya wagonjwa wanafika katika vituo vya afya kila mwezi wakilalamikia maumivu wakati wa kukojoa, haja ndogo ya mara kwa mara, uchafu au harufu mbaya ya mkojo, na hata homa kali. Wengi wa waathirika hawa hupata maambukizi yanayosababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli (E. coli), ambaye ameonekana kuhusika na zaidi ya asilimia 80 ya maambukizi ya njia ya mkojo duniani kote.  Hali hii imekuwa ya kurudiarudia kwa baadhi ya wagonjwa, na hivyo kusababisha adha ya kudumu inayohitaji matibabu ya mara kwa mara, na kwa baadhi, mpaka vipimo vya maabara kama Culture and Sensitivity ili kupatikana dawa sahihi. E. coli: Bakteria wa kawaida anayesababisha tatizo kubwa. Kwa kawaida, E. coli ni bakteria anayeishi kwenye utumbo wa binadamu bila madh...

Tarura Yashiriki Maonesho ya Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma

#Yajipanga kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu ushiriki wa vikundi vya kijamii katika matengenezo ya barabara nchini Dodoma  Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inashiriki Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni jijini Dodoma.  TARURA inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kazi na majukumu yake pamoja na kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TARURA Bi. Catherine Sungura amesema kuwa TARURA imejipanga kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wanayoyasimamia yanayohusu ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini. Kwa mujibu wa Bi. Sungura baadhi ya maeneo hayo ni pamoja usimamizi wa matengenezo ya kawaida, matengenezo ya maeneo korofi shughuli za maabara,mazingira na jamii. "Kupitia wataalamu wetu ambao wapo katika banda letu  tumejipanga pia kutoa elimu kwa wananchi na wadau wetu wengine namna wanavyoweza kushirikiana na TARURA kuwezesha m...