Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemuagiza Waziri wa Kilimo kukutana na wadau wa zao la pamba na ndani ya mwezi mmoja kuwasilisha mapendekezo ya mfumo bora wa ununuzi wa pamba utakaowanufaisha wakulima na kuendeleza uzalishaji wa zao hilo. Ametoa agizo hilo leo, Jumatatu Septemba 14, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Itilima, mkoani Simiyu, baada ya Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Daudi Silanga, kueleza changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba, ikiwemo malalamiko kuhusu mfumo wa sasa wa ununuzi. “Leo tarehe 14, mpaka tunapofika tarehe 14 mwezi ujao, niwe nimeshapata taarifa ya utaratibu mzuri ambao tutakubaliana,” amesema Dkt. Mwigulu. Amesema Serikali italinganisha mifumo iliyowahi kutumika na unaotumika sasa ili kupata utaratibu utakaokuwa na manufaa zaidi kwa wakulima bila kuathiri uzalishaji, bei ya pamba na maisha ya wananchi. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imeondoa sheria iliyokuwa ikiruhusu mifugo ya wananchi kutaifishwa na kuelekeza mapitio ya sh...
Marato tv - Sauti ya Jamii