-Nyumba 2,500 Zakamilika Msomera,Usambazaji wa Umeme Wafikia asilimia 98,Miundombinu Mingine Mbioni Kukamilika. Kassim Nyaki, Msomera Tanga. Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) tarehe 21 Novemba, 2024 imefanya ziara ya kikazi kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro wanaoendelea kuhamia eneo hilo. Akiongoza bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) amezipongeza Sekta zote zinazohusika kutekeleza mradi huo kijiji cha Msomera kwa kukamilisha Nyumba 2500, ujenzi wa miundombinu ya Maji, mawasiliano, barabara, minada, majosho, kituo cha kuuzia maziwa, shule, zahanati, shule, kutenga maeneo ya malisho na miundombinu mingine kijijini hapo. "Tumetembelea eneo la Block F ambapo nyumba 1,000 zimekamilishwa katika awamu ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa Nyumba 5,000, kitalu hiki pekee kuna matenki matatu ya maji yeny...
Marato tv - Sauti ya Jamii