Fresha Kinasa. Mara. NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesaema kuwa, serikali inalenga ifikapo mwaka 2030 kaya Mil. 15 ziwe zinatumia Kilimo mseto hapa nchini. Kitandula ameyasema hayo Novemba 14, 2023, wakati akifungua maonesho ya tisa ya Kilimo mseto yanayofanyika katika Kata ya Bweri Manispaa ya Musoma kuanzia Novemba 14, hadi Novemba 16, 2024. Ambapo yanawaleta pamoja wadau mbalimbali wa Kilimo mseto kutoka serikalini, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla. Amesaema kuwa, Wadau wa mazingira na Kilimo mseto wanalojukumu la kushirikiana katika utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa Kilimo mseto uliozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania machi 2024, huko Same Mkoani Kilimanjaro. Ambapo, Wizara ya Maliasili na Utalii ndio msimamizi wa mkakati huo, unaolenga kuhamasisha Kilimo mseto katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, lishe bora pamoja na kukuza kipato. Huku akiweka wazi kwamba, ...
Marato tv - Sauti ya Jamii