Skip to main content

Posts

Showing posts from August 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. MSEMO: SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE INAONGOZA TANZANIA

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dkt. Diwani Msemo, amesema saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayoongoza kwa wanawake nchini Tanzania, ikiwa pia miongoni mwa saratani zinazochangia vifo kwa kiwango kikubwa. Dkt. Msemo amesema takribani asilimia 34 ya saratani zinazowapata wanawake nchini ni saratani ya shingo ya kizazi, akisisitiza kuwa hali hiyo inapaswa kuchukuliwa kwa uzito kutokana na ukweli kwamba ugonjwa huo unaweza kuzuilika na kugundulika mapema. Amesema saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuzuilika kupitia chanjo, huku uchunguzi wa mara kwa mara ukisaidia kugundua mabadiliko ya awali na kutoa matibabu kabla ugonjwa haujawa mkubwa. “Ni saratani ambayo inaweza kuzuilika kwa chanjo, inaweza kugundulika mapema kupitia uchunguzi na inapogundulika katika hatua za awali, uwezekano wa kupona huwa mkubwa sana,” amesema Dkt. Msemo. Amesema hali hiyo inapaswa kuwa changamoto kwa jamii, kwa kuwa kuna wanawake wanaopoteza maisha kutokana na ugonjwa ambao kwa...

DKT. MSEMO: SARATANI INATIBIKA, HASA INAPOGUNDULIKA MAPEMA

  WANANCHI wametakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara na kutafuta huduma za kitabibu mapema, kwa kuwa saratani inaweza kutibiwa kwa ufanisi zaidi inapogundulika katika hatua za awali. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dkt. Diwani Msemo, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, Agosti 19, 2026, jijini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa wananchi kuondokana na dhana potofu kuhusu saratani na kuchukua hatua za mapema katika afya zao. Dkt. Msemo amesema wananchi wanapaswa kufahamu kuwa saratani si ugonjwa usiotibika, hasa pale inapogundulika mapema, huku akiviomba vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na ORCI kutoa elimu sahihi kwa umma kuhusu kinga, uchunguzi na matibabu ya saratani. Katika hatua nyingine, Serikali imeongeza uwekezaji mkubwa katika huduma za saratani kupitia ORCI, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza uwezo wa uchunguzi na matibabu, kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri huduma na kuimarisha nafasi ya ...

WIKI YA ELIMU YAZINDULIWA TANGA: SERIKALI YAMWAGA TRILIONI 2.8, BUNGE LATAKA BUNIFU ZIZALISHE PESA

Na MASHAKA MHANDO,Tanga Serikali imetangaza dhamira yake thabiti ya kuleta mapinduzi ya elimu ya ujuzi na ubunifu nchini, huku ikibainisha kuwa imetenga kiasi cha Shilingi Trilioni 2.8 kwenye bajeti ya Wizara ya Elimu ili kutekeleza kwa vitendo maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuandaa vijana kwa soko la ajira la ndani na nje ya nchi. Hayo yamebainishwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, wakati akizindua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika viwanja vya Usagara jijini Tanga, yakishirikisha zaidi ya taasisi na vyuo vikuu 90. Waziri Mkenda amesema mabadiliko makubwa yanayoendelea katika mitaala ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari za amali na vyuo vya VETA kila wilaya, ni matokeo ya maelekezo ya Rais Samia ambaye tangu aingie madarakani aliweka mkazo kwenye elimu inayojenga ujuzi. "Hiki mnachokiona kwa vijana wa Tanga Tech ni matokeo ya utekelezaji wa maono ya Rais. Hapo baadaye vizazi vijavyo vi...

SERIKALI KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Na. Mwandishi Wetu - Shinyanga SERIKALI imesema itaendelea kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), kwa kuboresha vituo vya huduma, kuwezesha vikundi na kuimarisha ushirikiano na wadau, ili kuhakikisha Tanzania inafikia lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dk. Jim Yonazi, wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga, ambapo alitembelea vikundi mbalimbali vya vijana vinaoishi na Maambukizi ya VVU pamoja na Kituo cha Maarifa Kahama kilichopo Kagongwa mkoani humo. Dk. Yonazi amesema juhudi zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau zimeanza kuzaa matunda, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza kasi katika utoaji wa elimu, upimaji, ushauri nasaha, pamoja na huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU. “Lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma karibu nao, lakini vilevile wanapata elimu inayowasaidia katika ma...

RC CHALAMILA ATOA SIKU SABA KUTAFUTA SULUHISHO LA MGOGORO WA ARDHI TOANGOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa muda wa siku saba kwa wananchi wa Toangoma, Wilaya ya Temeke, wanaodaiwa kuvamia eneo linalomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kutafakari na kutafuta ufumbuzi wa haraka ili pande zote ziweze kufikia hatua ya kupata haki kutokana na mgogoro huo.   Hayo ameyabainisha mapema leo, Agosti 19, 2026, katika mkutano na wananchi wa eneo hilo mara baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa wananchi, uongozi wa NSSF na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi. Katika mkutano huo, ilibainika kuwa eneo hilo ni mali ya NSSF, hivyo Mkuu wa Mkoa amesisitiza umuhimu wa kutafuta suluhisho la kibinadamu ili kutatua mgogoro huwo. Aidha Chalamila amewataka wananchi hao kuwa waungwana kwa kutambua chanzo cha mgogoro huwo n kutumia njia za kuzungumza badala ya kufikishana katika mamlaka za kisheria inaweza kuumiza baashi ya wananchi kutokana na uhalali wa viwanja hivyo.   Kwa upande wa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Reh...

DC CHIKOKA AJA NA MKAKATI KABAMBE KUINUA ELIMU MUSOMA WAZAZI KUSHIRIKISHWA.

Na Mwandishi wetu Jovina Massano Mkuu wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara Juma Chikoka aja na mkakati wa kuinua elimu mpango ambao utashirikisha wazazi utakaowezesha safari salama ya elimu kwa wanafunzi lengo ni kuwajengea uelewa na kuongeza ufaulu wilayani hapa. Akiongea katika kikao kazi cha tathmini ya elimu na viongozi wa Manispaa ya Musoma kilichowahusisha maafisa elimu,wenyeviti wa mitaa watendaji wa mitaa na Kata,maafisa maendeleo, vyombo vya ulinzi na usalama,waratibu elimu kata,madiwani,mstahiki Meya,Naibu Meya akiwemo na Mbunge wa Jimbo la Musoma.  Ameelezea kuwa mpango mkakati huo utakwenda kuchochea Maendeleo ya elimu kwa wanafunzi na kuongeza ubora wa elimu. " Ushiriki wa wazazi/walezi na wadau wote  ni muhimu katika safari ya elimu kwa wanafunzi kwa kuwa itasaidia kuongeza uelewa na ufaulu mzuri",amesema Chikoka. Mpango huo unatokana na taarifa ya hali ya elimu ya awali na msingi iliyotolewa na kaimu afisa elimu wa Manispaa ya Musoma Pendo Tongora ikielezea changamo...

COSTECH KUWASHIKA MKONO WABUNIFU.

Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) kuwasaidia wabunifu kuweza kufikia malengo yao,kuwezesha watu kupata ajira kupitia bunifu na kusaidia taifa kupata teknolojia mpya kupitia mashindano ya ubunifu na teknolojia. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa tume hiyo Prof. John Kondoro alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari siku ya uzinduzi wa maonesho ya wiki ya elimu ujuzi na ubunifu . Prof. Kondoro amesema kuwa mashindano ya ujuzi na ubunifu yanafaida kubwa katika kuhamasisha na kuendeleza bunifu mpya nchini sambamba na kuwezesha bunifu mbalimbali. Ilikufanikisha hayo yote Prof. Kondoro amesema COSTECH haifanyi kazi peke yake bali hushirikiana na taasisi nyingine zinazohusika na utafiti,ubunifu na teknolojia kama vile taasisi ya elimu ya juu,VETA, DIT na nyinginezo ili kuwasaidia wabunifu kukuza na kuendeleza mawazo yao. COSTECH pia Ina mfuko Kwa ajili ya kuwawezesha kifedha wabunifu ili kuweza kufika sokoni kwani waliowengi hushindwa kutimiza m...

VIKUNDI VYA CBRM VYATAKIWA KUWA WALINZI WA BARABARA ITILIMA ‎

  ‎Itilima, Simiyu ‎Vikundi vya kijamii vinavyotekeleza matengenezo ya kawaida ya barabara kupitia Mpango wa CBRM unaotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) vimetakiwa kushirikiana na wananchi katika kulinda na kutunza miundombinu ya barabara ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa jamii. ‎ ‎Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Anna Gidarya wakati wa mafunzo yaliyowakutanisha jumla ya vikundi 16 kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza kwa ufanisi shughuli za matengenezo madogo madogo ya barabara katika maeneo yao. ‎ ‎Mhe. Gidarya amesema barabara ni mali ya wananchi na ni sehemu muhimu ya kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii hivyo amewataka wanavikundi pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kuzilinda dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu hiyo. ‎ ‎Aidha, amevipongeza vikundi hivyo kwa kupata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika matengenezo ya barabara akieleza kuwa hatua hiyo si tu ina...