MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AFUNGUA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA UREKEBISHAJI KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII
Na. Ssgt Mawazo Mtondo - Dodoma. Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, leo Juni 10, 2026, amefungua rasmi Mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu Mwongozo wa Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji katika Ukumbi wa Rugimbana, Msalato, jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, CGP Katungu aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa namna inavyoendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Alisema Serikali imekuwa ikitoa rasilimali fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya magereza, makazi ya watumishi, vyombo vya usafiri pamoja na kugharamia mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa Jeshi la Magereza. CGP Katungu alibainisha kuwa moja ya majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza ni urekebishaji wa wafungwa kwa kuwapatia elimu, ujuzi na maarifa ili wanapomaliza vifungo vyao warejee katika j...