Skip to main content

Posts

Showing posts from April 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

CRJE launches Peninsular Noble Centre Building worth U$40million in Tanzania’s Business Capital

By Staff Writer The CRJE Investment (EA) has on Tuesday April 1, 2025 launched an exceptional commercial property, the Peninsular Noble Centre worth U$40million in Tanzania’s business capital of Dar es Salaam that flexible for Banks, supermarkets, coffee Bar, shops, and restaurants. “We have launched Peninsula Noble Centre, a commercial property, located in Oysterbay, Dar es Salaam, offering spaces for sale or rent, including supermarkets, Banks, Coffee Bar and shops” CRJE CRJE Investment (EA) General Manager Mr Li Tianye said. Tianye also said that so far, a number of clients have shown up for opening businesses, including banks, restaurants, supermarkets, and many more. On her part, the CRJE Investment (EA)’s Marketing Director Liu Dan said that Peninsula Noble Centre provides the ideal setting with state-of-the-art facilities and a vibrant commercial hub. “CRJE Investment (EA) started implementing this project in 2019, but we failed to continue due to the eruption of COVID 19. We st...

Dkt. Biteko Ashiriki Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Pwani

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 2, 2025 Kibaha mkoani Pwani katika viwanja vya Shirika la Elimu ameshiriki katika sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani humo. Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango. Sherehe hizo zilizoongozwa na kauli mbiu: “ Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu” zimehudhuriwa na viongozi  mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa. Viongozi wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu, Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Mzee Joseph Butiku.... Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya MNF

Uchaguzi...... Oktoba,uchaguzi mkuu ni jambo la katiba kila baads ya miaka mitano,Watanzania wenye sifa za kisheria kuruhusiwa kupiga kura, Sasa ubushi huu hata mimi nimeusikia,kama hakuna sheria za uchaguzi basi uchaguzi usiwepi Huo ni ubishi,vinabishana vyama vya siasa vipo kwa kw mujibu wa katiba,mambo ya siasa nchi kuongozwa na vyama na vina viongozi na vina wanachana.....huo ni ubishi,wanabushana kuhusu utaratibu wa kufanya jambo,Ni kitu gani kinafanya watanzania wanyang'anywe haki yao ya kupiga kura na miaka mitano imefika Huu ubishi si mzuri kwa wakati huu,kama hatutachagua lazima tuwe na serikali ambayo si halali Kuwa na serikali iliyochaguliwa...Watanzania waruhusuwe kupiga kura,hiyo nafasi isizuiwe lazima watanzania waruhusuwe kupiga kura Watu warusiwe katika uhuru wapige kura Rushwa,wagombea wanatos rushwa,nashauri watanzania wachukue pesa kisa wawanyime kura Kudai serikali inatimia mabavu Ubishi usimamizi ni watu gani.....walimu, Yoyote atakayeruhusiwa kusimamia...kwa n...

Nchimbi Atua Masasi Kuelekea Tunduru

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametua Uwanja wa Ndege wa Masasi, mkoani Mtwara, akiwa safarini kuelekea Tunduru, mkoani Ruvuma, tayari kuanza ziara yake ya siku 5. Uwanjani hapo, Balozi Nchimbi amepokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara, Ndugu Saidi Musa Nyegedi.

Kampuni ya CRJE kutoka China yazindua Jengo la biashara Peninsular Noble Centre jijini Dar

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya  CRJE Investment (EA) kutoka nchini China imezindua jengo jipya la kibiashara, Peninsular Noble Center ambalo limejengwa kwa thamani ya Dola za Kimarekani milioni 40 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuchochea uchumi wa nchi. Jengo hilo ambalo lipo Oysterbay, jijini Dar es Salaam lilianza kujengwa mwaka 2019 ni maalumu kwa maduka makubwa (supermarkets) na lina nafasi za ofisi, maeneo ya mazoezi na migahawa. "Tumezindua jengo letu la Peninsula Noble Centre hapa Oysterbay, Dar es Salaam ambapo tumeshaingia katika mikataba na baadhi ya Mabenki, supermarkets na migahawa ambapo watafungua ofisi zao hapa katika jengo hili la kibiashara,” Meneja Mkuu wa Kampuni ya CRJE Investment (EA) Bwana Li Tianye alisema. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa CRJE Investment (EA) Liu Dan alisema kuwa jengo la Peninsula Noble Center lenye mazingira bora ya kibiashara lilianza kujengwa mwaka wa 2019 lakini walishindwa kuendelea kutokana na mlipuko wa COVID-19. lakini wal...

Waziri Simbachawene Amtembelea Alhaj Songambele

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene, akitoa pole kwa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Tanzania Alhaj Mustafa Songambele Alipo mtembelea katika Hosptali ya Agakhan,Leo Aprili 2 Jijini Dar-es-Salaam. Ikumbukwe Alhaji Mustafa Songambele Aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam.

Makamu wa Rais Amesema Serikali Zote Zote Mbili Zinazingatia Haki za Msingi Kwa Wananchi Kushiriki Katika Uchaguzi Mkuu

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kusimamia kwa dhati na kwa haki misingi ya demokrasia na kuhakikisha wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi kwa uhuru, kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuchagua viongozi wenye sifa wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka  2025. Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani. Ametoa wito kwa wananchi wote hususan vijana kuwa waangalifu na watu wasioitakia mema nchi kwa kuepuka kutumiwa vibaya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani. Makamu wa Rais amesema Wadau wote wa uchaguzi, hususan vyama vya siasa wanahimizwa na kukumbushwa kuwa wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika katika hali ya amani na utulivu, kwa kuendesha kampeni zenye s...