Skip to main content

Posts

Showing posts from August 15, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhe. Vedastus Mathayo Akabidhi Zawadi Kwa Ajili ya Mathayo Polisi Jamii Cup Msimu wa 2024

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo leo agosti 15 amekabidhi ng'ombe, mipira 16 na fedha kiasi cha shilingi laki 2 kwa ajili ya mashindano Mathayo Polisi Jamii Cup 2024. Ng'ombe,mipira na fedha imekabidhiwa kwa mkuu wa polisi wilaya ya Musoma kama sehemu ya zawadi kwenye mashindano hayo yanayoyarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kushirikisha timu Kutoka Kata 16 za manispaa ya Musoma. Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya mbunge huyo Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo amesema huu ni mwaka wa pili ana dhamini mashindano hayo kwa lengo la kuwaweka vijana pamoja na kuinua viwango vyao. Amesema mbunge Mathayo ni mwanamichezo ambaye baada ya kuombwa na Jeshi la polisi wilaya ya Musoma kuwa sehemu ya kufanikisha mashindano hayo hakusita. " Mheshimiwa mbunge ameenda kwenye vikao vya bunge na ameniagiza nikabidhi mipira na ng'ombe kama zawadi kwenye mashindano ya Mathayo Polisi Jamii Cup. Ng'ombe itakuwa zawadi ya bingwa wa mashindano n...

Rais Samia Awasili Zimbabwe Kushiriki Mkutano wa 44 wa SADC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe kwa ajilli ya kushiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Harare nchini Zimbabwe tarehe 15 Agosti, 2024. Katika mkutano huo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya SADC.

Farida Joel Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji Halmashauri ya Mji wa Tarime

  Na Helena Magabe -Tarime Diwani wa Kata ya Kenyamanyori Mhe Farida Joel amechagulia kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira kwa mwaka 2024 ni baada ya kufanyika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti pamoja na kamati ndogo ndogo. Kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti kwenye kamati hiyo huwenda kile kilio chake cha  muda mrefu cha uchafu kutelekezwa kwenye mtaa wa kibaga mine kikaisha Kwa sababu idara ya afya iko chini ya kamati hiyo ya  mipango miji na mazingira hali kadharika Tarura.  Kabla ya Mheshimiwa huyokuchanguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo amehoji uchafu utaendelea kuishi kwenye mtaa wa kibaga mine hadi lini na mtaa huo utafikiwa lini na gari la taka  kwani imekuwa kero ya muda mrefu ambayo amekuwa akiilalamikia bila kupata majibu ya kina. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Nyamisangura amechaguliwa tena kuendelea kubaki kuwa Makamu Mwenyekiti huku Kata yake ikiwa na kero sugu ya dampo lilipo katikati ya makazi y...

Mkuu wa Majeshi Kuandika Historia Mpya Kwenye Mashindano ya Ngoma za Asili na Muziki wa Dansi

  Wakati mashindano ya mkuu wa majeshi Generali John Jacob Mkunda, yakitarajia kuanza Aug.19 mwaka vikundi mbalimbali vya utamaduni na muziki wa dansi vimeanza kujifua vikali huku kila mmoja akijinasibu kuondoka na ushindi katika mashindano hayo. Mashindano hayo ya kwanza nchini yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa jeshi wa Msasani Beach Club yanalenga kuhuisha tamaduni na muziki wa dansi ambao umeanza kutoweka kwa miaka ya hivi karibuni. Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufunguliwa ma waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Damasi Ndumbaro, yatahusisha vikundi kumi vya muziki wa Dansi na tisa vikiwa vikundi vya ngoma za asili. Waandishi wa habari wakiwa katika maeneo ya chuo cha mafunzo ya muziki na Sanaa cha jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania eneo la Mwenge,wameshuhudia kikundi cha utamaduni cha ngoma cha Mwenge Cultural kikijifua vikali kwa huku nyimbo na tambo mbalimbali zikisikika hali inayoashiria maandalizi mazuri kuelekea mashindano hayo. Nako kwenye muziki wa dansi k...