Skip to main content

Posts

Showing posts from November 17, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Madini Yaibuka Kama Nguzo ya Maendeleo Morogoro

🔶 Sekta yaongezeka kwa kasi, yajenga miundombinu na kuinua wananchi Morogoro Mauzo ya madini ya dhahabu mkoani Morogoro yamefikia Shilingi bilioni 16.51 katika kipindi cha Julai 2023 hadi Septemba 2025, yakionesha kasi kubwa ya ukuaji wa sekta ya madini na mchango wake katika uchumi wa mkoa. Mapato ya Serikali kupitia sekta hiyo pia yameendelea kupanda kutoka Shilingi bilioni 2.67 mwaka 2021/2022 hadi Shilingi bilioni 4.9 mwaka 2023/2024, huku Morogoro ikitarajia kukusanya Shilingi bilioni 6.5 katika mwaka wa fedha 2025/2026. Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Morogoro inasimamia shughuli za madini katika wilaya za Gairo, Kilosa, Mvomero na Morogoro. Akizungumza katika mahojiano maalum, hivi karibuni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Zabibu Napacho, alisema kuwa mkoa huo umebarikiwa na aina nyingi za madini ikiwemo Feldspar, Rhodolite Amethyst, Green Garnet, Dhahabu, Kaolin, Shaba, Ruby, Spinel, Marble, Graphite, REE na Quartz. Alifafanua kuwa jumla ya leseni za uchimbaji mdogo zilizoto...

Dkt. Mwigulu Akabidhiwa Ofisi Rasmi

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Novemba 17, 2025 amekabidhiwa Ofisi na  Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa, Mlimwa Jijini Dodoma Novemba 17, 2025.  Viongozi waliohudhuria hafla ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Doto Biteko, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa Idara na watumishi wengine wa Ofisi ya Waziri Mkuu.