Skip to main content

Posts

Showing posts from December 10, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Paja la Nyama ya Mbuzi 5,000 Mitaani Mwanza

 Mwananchi wa Jiji la Mwanza wako katika hatari kubwa baada kundi la watu kukutwa katika mtaa wa Liberty zikiuwaza ovyo na baadhi ya watu. Nyama hizo zinauzwa kwa mafungu huku paja kubwa likiuzwa shilingi 5000 jambo ambalo linatia mashaka kama nyama hizo ni salama kwa matumizi ya binadamu.  Baadhi ya watu wakiwemo baadhi ya Mama ntilie wameonekana kununua kwa wingi nyama hizo.

Arusha Wamshukuru Rais Samia Kwa Nishati safi ya Kupikia

📌Majiko ya Gesi ya Ruzuku yawafikia  Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya 50% katika halmashauri hiyo. Wametoa pongezi hizo Desemba 10, 2024 wakati wa utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo. Walisema mradi huo umefika wakati mzuri kwani kwa sasa upatikanaji wa mkaa ni mgumu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na hii inasababisha kupanda kwa gharama za maisha. "Tumefurahi kufikiwa na mradi, suala la kuni na mkaa hapa kwa sasa ni shida; tunatumia muda mrefu kuwasha moto maana kuni ni mbichi," alisema Neema Rumas mkazi wa kijiji cha Siwandeti. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Siwandeti, Daniel Mitiweki amesema ujio wa mradi huo ni mkombozi wa mazingira kwani suala la ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na...

Aliyekuwa Rais wa Zambia Edgar Lungu agonga Mwamba Kuwania Tena Urais

Mahakama ya Katiba nchini Zambia imetoa maamuzi  kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Edgar Lungu hawezi kuwania tena kiti cha Urais kwenye  uchaguzi wa mwaka 2026 kwa kuwa tayari amehudumu mihula miwili. Mahakama hiyo imeamua kuwa muda ambao Lungu alihudumu kama Rais wa taifa hilo kuanzia mwaka 2015 hadi 2021 kufuatia kifo cha Michael Sata aliyekuwa madarakani, kinahesabiwa kama mihula miwili.

Wakinamama Chalinze Wampa Tano Rais Samia Kwa Nishati Safi

Maneno haya yamesema na Bi. Lilian Skawa kwa niaba ya wakinamama wa Chalinze mbele ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze na WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Wenye Ulemavu Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati wakipokea  majiko ya gesi 118 kwa mama lishe wa kata 15 za Jimbo la Chalinze.  Ndg. Ridhiwani  Kikwete amesema lengo kubwa la kugawa majiko haya ya gesi ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika  kutunza mazingira na kuwafanya wananchi kuondokana na matumizi ya nishati chafu. " Sasa mtakwenda kupika chakula kwa haraka na kwa Usafi na hii itasaidia katika shughuli zenu kwa pamoja tutamuunga Mhe. Rais  kwenye uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambayo italinda afya zenu pia" amesema Afisa Maendeleo ya Jamii na mratibu wa dawati la Jinsia wa Halmashauri hiyo Recho Mnguruta amesema  majiko hayo yatakwenda kuwasaidia Wanawake wajasiriamali hao kuondokana na  kutumia kuni na mkaa. Naye Bi. Lilian Skawa mkazi wa Msata ...

Mradi wa Inclucities Waja na Suluhishi la Ukosefu wa Ujusi Miongoni Mwa Wasomi

  Ukosefu wa Ujuzi Miongoni mwa baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu pamoja na vya kati nchini umetajwa kuwa kikwazo kwa baadhi yao katika kupata ajira kwenye sekta binafsi. Hatua hiyo inafuatia baadhi ya waajiri kutotoa nafasi za ajira baada ya kubaini kuwa baadhi ya wahitimu hawana ujuzi unaohitajika katika kuwawezesha kuongeza tija kwenye shughuli zao za uzalishaji mali. Hayo yamebainishwa Jijini mwanza na Mshauri Mtaalam wa masuala ya ujengaji ujuzi kwa vijana kwenye Mradi wa Inclucities Thomas Aikaruwa wakati wa kikao baina ya baadhi ya  waajiri pamoja na vyuo vinavyotoa mafunzo ya ujuzi na ufundi stadi mkoani mwanza kilicholenga kutafuta suluhisho la tatizo la ukosefu wa ujuzi miongoni mwa wahitimu wa fani mbalimbali. ‘’Kuna vijana wengi tunao mtaani ambao wanatafuta ajira lakini pia tunao waajiri wanaotafuta vijana wenye ujuzi unaohitajika kwenye maeneo yao ya kazi,kwa hiyo kumekuwa na pengo  hilo kati ya waajiri na waajiriwa,kwa hiyo tumeamua kuwakutanisha pande zote ...

Tuendelee Kutumia Teknolojia katika Shughuli za Uhifadhi-Dkt. Abbasi

Na. Joyce Ndunguru, Morogoro Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi ameelekeza kuendelea kwa matumizi ya teknolojia mbalimbali katika ulinzi wa rasilimali ya wanyamapori. Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Disemba 10, 2024, katika kikao na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kilichofanyika katika Makao Makuu ya TAWA Mkoani Morogoro. "Tuendelee kutumia teknolojia za kisasa katika ulinzi wa rasilimali ya wanyamapori ", amesema Dkt. Abbasi. Aidha, Dkt. Abbasi ameipongeza TAWA kwa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma mnamo mwezi Septemba ya kununua ndege nyuki kwa ajili kudhibiti wanyama wakali na waharibifu. "Nimefurahi kuona mmeanza kutekeleza maelekezo ya Rais ya kununua ndege nyuki na hapa TAWA nimeona kazi imeanza" ameongeza Dkt. Abbasi Vilevile, Dkt. Abbasi alitoa pongezi kwa TAWA kwa ujenzi wa vizim...