* Waganga wafawidhi, wafamasia wapigwa msasa kuzuia uchepushaji Na MASHAKA MHANDO, Tanga MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imetoa mafunzo maalum kwa Waganga Wafawidhi, Wafamasia na Wakaguzi wa dawa kutoka wilaya nne za Mkoa wa Tanga, lengo likiwa ni kudhibiti matumizi holela ya dawa za tiba zenye asili ya kulevya (Narcotics & Psychotropics) ili kuzuia uraibu miongoni mwa vijana. Mafunzo hayo yaliyolenga wilaya za Tanga Jiji, Muheza, Pangani na Mkinga, yanakuja kama mkakati wa Serikali kuhakikisha dawa hizo kali ambazo ni muhimu kwa wagonjwa wa upasuaji na saratani, haziingii mitaani kinyume cha sheria. Akizungumza katika mafunzo hayo, Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki, Keddy Manga, alisema kuwa jukumu la msingi la mamlaka hiyo ni kuhakikisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi ni bora, salama na vina ufanisi, lakini tahadhari kubwa inahitajika kwenye dawa za maumivu makali. “Kuna dawa zinatumika kwa wagonjwa wenye maumivu makali kama wa saratani au wanaofanyiwa upasuaji. Hata hivy...
Marato tv - Sauti ya Jamii