Kamati ya Huduma za Kiuchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, imeridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.1, iliyotembelewa na kukaguliwa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Salehe Jumanne Salehe, amepongeza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, inakidhi viwango vinavyotakiwa na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi. Mhe. Salehe amewataka wataalamu wa halmashauri kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo zinapangwa na kutengwa kwa wakati, kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa katika mipango na bajeti ya mwaka husika. Amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuondoa ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi na kuwezesha shughuli za ujenzi kuendelea kulingana na ratiba zilizopangwa. A...
Marato tv - Sauti ya Jamii