Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka Mawakili na Maafisa Sheria wa Serikali kuhakikisha sheria, mikataba na maamuzi ya Serikali vinalinda uhuru, usalama, rasilimali na maslahi ya Taifa. Rais Dkt. Samia ametoa agizo hilo leo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA). Amesema ushindani wa kiuchumi na kisiasa duniani unaitaka Tanzania kuwa na mfumo imara wa sheria unaolinda mamlaka ya nchi, uchumi wake na rasilimali za Taifa. Aidha, amewataka Mawakili wa Serikali kutambua vihatarishi vya kisheria mapema na kutoa ushauri kabla ya Serikali kuingia mikataba, kuanza miradi au kufanya maamuzi makubwa ili kuepusha hasara inayoweza kutokea kutokana na maamuzi hayo. "Ni wajibu wenu kugundua vihatarishi mapema, kushauri kwa wakati na kuhakikisha nchi inalindwa kwa misingi imara ya kisheria," amesema Rais Dkt. Samia. Halikadhalika, amesisitiza ushirikishwaji wa Mawakili na Maa...
Marato tv - Sauti ya Jamii