Na Shomari Binda-GMTV MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amepongeza maendeleo ya kielimu yanayofanywa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo. Pongezi hizo amezitoa Mara baada ya mbunge huyo kushusha mbao zaidi ya 2000 zitakazoendeleza mradi wa utengenezaji wa madawati,viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kukalia. Akizungumza na GMTV amesema hakuna jambo na urithi ulio bora kama elimu hivyo juhudi za mbunge huyo zinapaswa kupongezwa. Amesema mwanafunzi anapopata sehemu nzuri ya kukaa na kupata elimu uzingatia kinachofundishwa akiwa darasani. Chikoka amesema kama mdau wa maendeleo yakiwemo ya elimu anapongeza juhudi zinazofanywa na mbunge Mathayo. Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewekeza kwenye elimu kwa ujenzi wa shule mpya na kuongeza madarasa ili watoto wapate elimu na mambo ya kumuunga mkono ni kama anavyofanya mbunge Mathayo. " Kwa sasa mzazi achangishwi fedha kwaajili ya ujenzi wa shule na madarasa kazi knafanywa Rais Dkt.S...
Marato tv - Sauti ya Jamii