Skip to main content

Posts

Showing posts from December 12, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wanawake Jimbo la Chalinze Wamshukuru Rais Dkt. Samia Kuwapatia Majiko ya Gesi

  Na Ghati Msamba. Wakinamama wa Jimbo la Chalinze wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuleta nishati safi, baada ya kupokea majiko ya gesi 118 yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ndg. Ridhiwani Kikwete, kwa mama lishe wa kata 15 za jimbo hilo. Taarifa hii ilitolewa katika hafla iliyoandaliwa katika ofisi ya Mbunge huyo, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria. Katika hotuba yake, Ndg. Ridhiwani Kikwete alisema kuwa lengo kuu la kugawa majiko haya ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kudumisha mazingira bora na kuhamasisha matumizi ya nishati safi, hasa kwa wanawake wajasiriamali ambao kwa kawaida hutumia kuni na mkaa kupikia. "Sasa mtakwenda kupika chakula kwa haraka na kwa usafi. Hii itasaidia kuboresha shughuli zenu na kuendelea kuunga mkono kampeni ya Rais Samia ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi," alisema Kikwete. Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Jinsia wa Halmashauri ya Chalinze, Bi. Recho Mnguruta, alieleza kuwa maji...

Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali Watu Serikalini Wakutana Kubadirishana Uzoefu

Na Hamida Ramadhan  Dodoma KAIMU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi amewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Serikalini kushiriki Kikao Kazi kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupata maelekezo kuhusu masuala yanayohusu Usimamizi wa Rasilimali watu katika utumishi umma kwa kuzingatia shabaha na vipaumbele vya Taifa.  Kaimu Katibu Mkuu huyo amebainisha hayo leo Alhamisi Desemba 12, 2024 wakati akizungumza na  Waandishi wa Habari jijini hapa kuhusu kikao kazi hicho kitakachofanyika Desemba 17-19, mwaka huu mbapo amesema Washiriki wa kikao hicho ni kutoka kwenye Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika na  Taasisi za Umma, Sekretarieti za Mikoa  na Serikali za Mitaa. Daudi amesema kupitia kikao hicho Wakuu hao watapata fursa ya  kubadilishana mawazo na maelekezo kuhusu vipaumbele vya serikali kwenye ajira, maandalizi ya ikama na bajeti ya mishahara kwa Watumi...

Miradi ya afya inayojengwa iendane na Thamani ya Fedha

Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini, kuhakikisha wanasimamia thamani ya fedha katika Miradi mbalimbali ya Afya inayotekelezwa katika maeneo yao ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa. Dkt. Grace amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya mpango wa uwekezaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto (TMCHIP) yaliyofanyika mkoani Morogoro  yakihusisha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, Wahandisi majengo, Maafisa Ugavi, Maafisa Mipango, Wahasibu, PPRA,Waratibu wa Miradi, Makatibu wa Afya na Waganga wafawidhi  kutoka katika mikoa 17 na Halmashauri 25 ambapo mradi  huo umeanza kutekelezwa. “Kila mtaalamu aliyehudhuria hapa akasimame kwenye nafasi yake, popote pale ambapo mradi utaharibika hakuta kuwa na visingizio hatua stahiki zitachukuliwa kwa sababu wote mpo hapa kama timu moja ya utekelezaji wa mradi huu, hivyo nasisitiza miradi hii ya ujenzi...

Waziri Mavunde kuzindua mnada wa vito Desemba 14 Mirerani,Manyara

  ▪️Waziri Mavunde kuzindua Mnada Rasmi ▪️Lengo ni kuyaongezea thamani ▪️Kudhibiti utoroshaji ▪️Kuuzwa kwa bei ya ushidani MANYARA: WAZIRI wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mnada wa madini ya vito unaotarajiwa kufanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, ili kuyaongezea thamani madini hayo. Mnada huo ambao ulisimama kwa muda, umepangwa kufanyika tena kwa mara ya kwanza Desemba 14, 2024. Akizungumza leo Desemba 12, 2024, Mheshimiwa Mavunde amesema madini ya vito, yanafanyiwa mnada kama mkakati wa kuyatangaza na kuyaongezea thamani kimataifa. Mheshimiwa Mavunde amesema utaratibu wa kufanya mnada huo ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia. Amesema, mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi na atakayenunua madini hayo katika mnada ni atakayeshinda bei iliyowekwa....

Tutaendelea kutatua changamoto za Walimu-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kutatua changamoto za walimu zikiwemo za malimbikizo ya madeni na upandishaji wa madaraja. Amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua, anathamini na kuheshimu kazi kubwa inayofanywa na walimu wote nchini katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kukuza na kuiendeleza sekta ya elimu nchini. Amesema hayo leo (Alhamisi, Desemba 12, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 19 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Jakaya Kikwete jijini Dodoma “Kwa sasa suala la stahiki za walimu linaendelea kuzingatiwa na Serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha inapadisha madaraja watumishi walimu waliokosa na wanaopaswa kupandishwa, Serikali imedhamiria kuondoa msamiati wa areas (malimbikizo ya mishahara).” Amesema kuwa k...

Bashungwa aagiza Malalamiko ya Wananchi Kufanyiwa Kazi na Mfumo wa Utoaji Taarifa Kuboreshwa

Na Mwandishi Wetu,DODOMA  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa (Mb) ameiagiza Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kusimamia Kitengo kinachoshughulikia Malalamiko yanayotolewa kwa Wizara, Taasisi na Vyombo vya Usalama kuhakikisha wanayafanyia kazi na kutoa mrejesho wa utatuzi wa malalamiko kwa Wananchi. Aidha, Bashungwa amevitaka Vitengo vya Mawasiliano na Habari vya Wizara, Vyombo vya Usalama na Taasisi zote kuboresha mfumo wa Mawasiliano na habari kwa umma. Ameeleza hayo leo tarehe 12 Disemba, 2024 wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba - Dodoma na kusisitiza kuwa ni haki ya Watanzania kupata  taarifa sahihi kwa wakati. “Kuna Malalamiko mengine yanakuwepo kwa sababu hamna taarifa sahihi au taarifa imechelewa, kwahiyo lazima mhakikishe mnashughulikia Malalamiko na kutoa mrejesho”, ameeleza Bashungwa.  Vilevile, Bashungwa ametoa wito kwa Watumishi wa Wizara kutoa ush...