Devotha Daniel Mburarugaba na Samira Khalfani Amour wameibuka washindi kati ya wagombea nane walioshiriki katika uchaguzi wa kura za maoni nafasi ya ubunge wa viti maaluma mkoa wa Kagera kupitia Umoja wa wanawake Tanzania (UWT). Akitangaza matokeo hayo,Msimamizi wa Uchaguzi huo mjumbe wa baraza kuu UWT Taifa Yasmin Bachu amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na wagombea nane, jumla ya wapiga kura walikuwa 1,483 ambapo kura moja ilihalibika hivyo kura halili zikiwa 1,482. Bachu amewataja Devotha Daniel aliyepata kura 1,308 na Samira Khalfani 1,250 kuwa wameongoza katika uchaguzi huo wakifuatiwa na Anitha Korongo kura 153,Elizabeth Ngaiza kura 94,Anitha Bunono kura 52,Anitha Nyamzinga kura 44,Herieth Lugaju kura 37 na Evastina Godian kura 26. Aidha Bachu amewashauri wajumbe wa UWT mkoa wa Kagera kuwa wakati wa kampuni za Dk.Samia Suluhu Hassan wapaze sauti kwa na kuunganisha nguvu za kumuombea kura zitoshe pia kushinda majinbo yote rb ya mkoa wa Kagera ili kuwawezesha washindi hao w...
Marato tv - Sauti ya Jamii