Skip to main content

Posts

Showing posts from April 29, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Wateta na Spika wa Bunge wakiwa Uwanja wa ndege

   Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakielekea Dodoma, leo tarehe 30 Aprili, 2026.

Pandeni Miti Yenye Tija -Mtaka

Alvin Mushi - Njombe  MKUU wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewataka wananchi  mkoani hapa kupanda miti yenye tija kama vile maparachiichi badala ya kupanda miti ya mapambo, Bw Mtaka, ametoa wito huo wakati wa zoezi la upandaji miti uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mei Mosi 2026 ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani hapa. Aidha amesema endapo kila mwananchi atapanda miti ambayo itamuongezea kipato kwanza atakuwa amekuza uchumi wake binafsi na taifa kuliko kuwa na miti ambayo faida yake ndogo. “Miparachichi  ndiyo habari ya mjini yana soko kubwa ndani na nje ya nchi unaweza kupanda hata kuzunguka nyumba yako na ukapata faida kuliko kuwa na miti mingi ambayo inaishia kuwa mapambo” amesema Bw Mtaka

Tamasha la kilimo lahitimishwa Mbeya

📌 *REA Yapongezwa uhamasishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia* . 📌 *Umeme sasa ni kitongoji kwa kitongoji*  📍 *Iwambi, Mbeya* . Tamasha la Kilimo lililokuwa likifanyika mkoani Mbeya limehitimishwa rasmi leo Jumatano, tarehe 29 Aprili 2026, kwa mafanikio makubwa huku likiwa limekusanya wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, nishati na maendeleo kutoka ndani na nje ya mkoa huo. Tamasha hilo limekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kuonesha teknolojia mpya na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu njia bora za kuboresha maisha yao kupitia kilimo na matumizi sahihi ya nishati. Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga tamasha hilo,mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu ameipongeza REA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya matumizi ya nishati safi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ina mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi na kulinda mazingira. Alieleza kuwa matumizi ya nishati safi kama majiko ya umeme, majiko ya gesi na majiko ba...

CPL Stella Lymo akabidhi Tuzo Kwa RPC Mutafungwa

Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza ​Koplo Stella Lyimo, mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Nyamagana, Mkoani Mwanza, amemkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza tuzo na vyeti alivyoipokea tarehe 25 Aprili 2026, katika hafla iliyofanyika leo, 29 Aprili 2026, katika Bwalo la Polisi Mabatini. ​Akipokea tuzo na vyeti hivyo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa, amesema kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuthamini na kutambua mchango wa kila askari anayefanya vizuri katika majukumu yake. Aidha, aliwataka askari wote kuongeza juhudi na nidhamu mahali pa kazi. ​"Ninawataka askari wengine kuwajibika kikamilifu kwa kuwahudumia wananchi na kulinda raia pamoja na mali zao kama inavyopaswa.Tunalenga kuwa na taasisi inayoheshimika na kupendwa na wananchi," alisema Kamanda Mutafungwa. Katika taarifa iliyosomwa mbele ya Kamanda Mutafungwa, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, SSP Virginia Sodoka, alibainisha kuwa Koplo Stella amekuwa akifanya kazi kwa umahiri mk...

Bangi: Zao Lenye Gharama Nafuu, Fursa Mpya kwa Uchumi wa Wakulima – Waitara

KATIKA mjadala unaozidi kushika kasi kuhusu mageuzi ya sekta ya kilimo, Mbunge wa Tarime, Mwita Waitara, ameibua hoja nzito akitaka Serikali kuanza kuangalia upya uwezekano wa kuruhusu kilimo cha bangi kama njia mbadala ya kuinua uchumi wa wakulima. MBUNGE Waitara ameibua hoja hiyo leo  April 29,2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati Akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo ambapo amesema kuwa tofauti na mazao mengi ya biashara, bangi ina gharama ndogo za uzalishaji kwani haihitaji matumizi makubwa ya mbolea wala pembejeo ghali.  Hali hii, kwa mujibu wake, inaweza kuwa mkombozi kwa wakulima wadogo wanaokumbwa na changamoto ya gharama kubwa za uzalishaji. “Tunahitaji kufikiria nje ya mfumo wa kawaida. Kuna mazao yenye tija kubwa na gharama ndogo ambayo yanaweza kuwainua wakulima wetu,” ameeleza. Mbali na mchango wake katika uchumi, Waitara ameangazia pia thamani ya bangi katika sekta ya afya, akibainisha kuwa imekuwa ikitumika katika matibabu ya baadhi ya magonjwa kama saratani na mata...

Mariam Ditopile Ashauri Mirungi Liwe zao la biashara

   MBUNGE wa Jimbo la Kondoa Mjini, Mariam Dittopile, ameitaka Serikali kufanya tathmini ya kina na kufungua mjadala mpana kuhusu uwezekano wa kuruhusu kilimo na biashara ya zao la mirungi Kwa  mfumo rasmi wa kisheria. Akichangia Bajeti ya wizara ya Kilimo leo April 29,2026 Bungeni Jijini Dodoma, Mhe.Mariam  Dittopile amesema ni wakati sasa wa kuacha mtazamo wa kupiga marufuku bila uchambuzi wa kutosha, badala yake kuangalia fursa za kiuchumi zinazoweza kunufaisha Taifa. Amesema kuwa nchi jirani zimekuwa zikivuna mapato makubwa kupitia zao hilo , huku Tanzania ikiwa haijatumia ipasavyo fursa iliyopo.  Aidha, Amesema Soko la mirungi lina mzunguko mkubwa wa fedha kimataifa, jambo linaloashiria uwepo wa chanzo kipya cha mapato iwapo kitawekewa mfumo sahihi wa usimamizi. “Tunapaswa kujiuliza kama tunawanufaisha wengine bila sisi kujua. Wakati wenzetu wanakusanya mamilioni ya dola, sisi bado hatujachukua hatua ya kisheria kulisimamia zao hili,” amesema. Ameishauri Se...

Bangi: Zao Lenye Gharama Nafuu, Fursa Mpya kwa Uchumi wa Wakulima – Waitara

KATIKA mjadala unaozidi kushika kasi kuhusu mageuzi ya sekta ya kilimo, Mbunge wa Tarime, Mwita Waitara, ameibua hoja nzito akitaka Serikali kuanza kuangalia upya uwezekano wa kuruhusu kilimo cha bangi kama njia mbadala ya kuinua uchumi wa wakulima. MBUNGE Waitara ameibua hoja hiyo leo  April 29,2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati Akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo ambapo amesema kuwa tofauti na mazao mengi ya biashara, bangi ina gharama ndogo za uzalishaji kwani haihitaji matumizi makubwa ya mbolea wala pembejeo ghali.  Hali hii, kwa mujibu wake, inaweza kuwa mkombozi kwa wakulima wadogo wanaokumbwa na changamoto ya gharama kubwa za uzalishaji. “Tunahitaji kufikiria nje ya mfumo wa kawaida. Kuna mazao yenye tija kubwa na gharama ndogo ambayo yanaweza kuwainua wakulima wetu,” ameeleza. Mbali na mchango wake katika uchumi, Waitara ameangazia pia thamani ya bangi katika sekta ya afya, akibainisha kuwa imekuwa ikitumika katika matibabu ya baadhi ya magonjwa kama saratani na mata...

Tanzania Yapongezwa kwa Mchango wa Madini kwenye Pato la Taifa

▪️Nchi za Kenya,Somalia na Sudani Kusini kujifunza maendeleo ya sektaya madini ▪️Rais Samia apongezwa kwa kukuza sekta ya Madini ▪️Rais Ruto azitaka nchi za Afrika Mashariki kuunganana kuongeza thamani rasilimali madini ▪️Waziri Mavunde akaribisha wawekezaji Tanzania 📍 Nairobi, Kenya Sekta ya Madini nchini Tanzania imeendelea kung’ara kimataifa baada ya kupongezwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza pato la taifa (GDP), huku nchi jirani zikieleza nia ya kujifunza mafanikio ya usimamizi wa sekta hiyo. Wakizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Madini (Kenya Mining Investment Conference and Expo -MICE) 2026, unaofanyika jijini Nairobi kwa siku mbili 28 hadi 29 Aprili 2026 MICE 2026 Nairobi, na kuhudhuriwa na Viongozi , Wawekezaji na Wadau wa Sekta ya Madini barani Afrika, Mawaziri mbalimbali Madin wa Afrika walitambua hatua kubwa zilizopigwa na Tanzania katika kuifanya sekta ya madini kuwa mhimili wa uchumi. Akizungumza katika mdahalo maalum wa mawaziri hao, Waziri wa Ma...

Mhe.Ghati Chomete Aibana Serikali;fedha za kilimo zitoke kwa wakati,Viwanda vifufuliwe

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Zephania Chomete, ameibana Serikali kuhakikisha fedha zilizoombwa na Wizara ya Kilimo zinatolewa kwa wakati ili kutekeleza miradi ya kilimo kwa ufanisi. Akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Aprili 28, 2026, katika Bunge la 13 jijini Dodoma, Mhe. Chomete alisisitiza kuwa bila uwekezaji wa kutosha, sekta ya kilimo haiwezi kuleta mageuzi yanayotarajiwa kwa wakulima. “Kilimo ni zaidi ya chakula; ni biashara na ajira. Tukikifadhili ipasavyo, tutainua maisha ya wananchi wetu.” Katika hoja yake, alielekeza pia umuhimu wa kufufua viwanda vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani na soko la uhakika kwa wakulima. Sambamba na hilo, aliitaka Serikali kudhibiti bei za pembejeo na mazao ili wakulima wanufaike na jasho lao. Mhe. Chomete amesisitiza pia kuwa hatua hizo zitachochea uzalishaji wenye tija, kuongeza kipato cha wakulima na kuimarisha uchumi wa Taifa.

Rais Ruto kulihutubia Bunge la Tanzania Mei Tano

 RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5, 2026, katika tukio linalotarajiwa kuvuta hisia za kisiasa na kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Akisoma tangazo rasmi la Katibu wa Bunge leo Aprili 29, 2026, Naibu Spika, Daniel Sillo, amesema kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, huku hotuba ya Rais Ruto ikipewa uzito mkubwa kama sehemu ya mjadala wa siku hiyo. Kwa mujibu wa Sillo, ujio wa kiongozi huyo unalenga kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya, hasa katika sekta za biashara, uwekezaji na maendeleo ya uchumi eneo ambalo limeendelea kuwa mhimili wa uhusiano wa nchi hizo mbili. Tangazo hilo limetolewa katika Kikao cha 19 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13 la Tanzania kinachoendelea jijini Dodoma. Hotuba hiyo inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuonesha dira ya ushirikiano wa kikanda na kufungua fursa mpya za maendeleo kwa mataifa haya jirani.