Na Angela Sebastian; Bukoba WAZAWA wa kijiji cha Buzi kata ya Buzi iliyopo Wilayani Bukoba mkoani Kagera wamewaomba wenzao walioko ndani na nje ya nchi kuondokana na wasiwasi wa imani za kishirikiana ambazo ziligubika kijiji hicho huko nyuma na kuja kuwekeza na kuleta maendeleo. Edwin Mugoha ni mwenyekiti wa umoja wa Wanabuzi waishio nje na ndani ya Tanzania (Buzi Development Community-BUDECO) ambapo amesema kwa kipindi cha miaka minne sasa wamedhamilia kuweka mkakati madhubuti wa kuunda chama ambacho kinaunganisha wanabuzi wa ndani na nje ili kurudi nyumbani na kuondoa fikra potofu kwa kukuza uchumi wa nyumbani kwao. Mugoha alisema hayo jana wakati wa madhimisho ya Buzi day ambayo imeadhimishwa kijijini humo na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali na watumishi wa Serikali,wadau kutoka maeneo mbalimbali na wanachama wenyewe. "Chama chetu chenye wanachama 60 wa kuanzia walioko ndani na nje ya nchi tumerudi nyumbani ili kuijenga Buzi yetu sisi wenyewe kwa kushirikiana na Se...
Marato tv - Sauti ya Jamii