Na Mashaka Mhando, Tanga Wanachama 158 wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mkoani Tanga wamejiondoa kwenye chama hicho kwa madai kwamba chama hicho kimepoteza muelekeo na hivi sasa kimekuwa chama cha matusi, kudharauliana na kukejeliana kwenye mitandao ya kijamii. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga Mjumbe wa Kamati ya mafunzo kanda ya Kaskazini Zainab Ashraf amesema kwamba wanaondoka katika chama hicho si kwamba wanamfuata aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe bali sababu zilizowafanya wajiondoe ni kutokana na kupoteza muelekeo wa chama hicho pamoja na kukosekana kwa demokrasia ya kweli. "Tunajivua rasmi uanachama wa Chadema tutatafuta jukwaa jingine kwasababu wengi wetu hapa ni wanasiasa bado tuna ndoto zetu za kisiasa hazijatimia tutapata jukwaa jengine ambalo tutaliona ni rafiki na sisi kuendeleza harakati hizi za kutafuta demokrasia ya kweli na mapambano ya kweli kuwaokoa watanzania katika jukwaa tutakaloliona ni rafiki, "ali...
Marato tv - Sauti ya Jamii