Skip to main content

Posts

Showing posts from October 24, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Madereva wa bodaboda watakiwa kuvaa kofia ngumu

 Na Dawati la Habari Polisi Mwanza Madereva wa boda boda watakiwa kuvaa kofia ngumu na kufata Sheria za usalama barabarani pindi wanapotumia pikipiki ili kuepukana na ajali ambazo zinaweza wapelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa.  Hayo yamebainishwa Oktoba 24.2024 na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza  Mrakibu wa Polisi (SP) Sunday Ibrahim wakati akitoa  elimu ya usalama barabarani kwa  waendesha boda boda wa vituo vya kata za Nyegezi, Luchelele na Mkolani wilayani Nyamagana mkoani Mwanza. Akizungumza na madereva wa boda boda hao kutoka kanda ya Mwanza kusini,Sunday amesema elimu hiyo  imelenga kuwapa uelewa makundi mengine ya watumiaji wa barabara  hususan bodaboda ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika. Aidha, SP Sunday amesema, atahakikisha operesheni inayoendelea haimuacha mtu ambapo watakaobaini kutovaa Korea ngumu kinyume cha sheria watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.  " wengi mnasema abiria hataki ...

Kikao cha 20 Bodi ya GST chafanyika chaongozwa na Prof.Ikingura

*Asisitiza juhudi na ubunifu kazini* Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Prof. Justinian Ikingura ameongoza Kikao cha 20 cha Bodi ya Taasisi hiyo ambapo ameitaka Menejimenti ya GST kuongeza juhudi na ubunifu katika ukusanyaji wa maduhuli ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali. Hayo ameyasema leo Oktoba 24, 2024 katika kikao cha Bodi ya GST kilichofanyika kwenye ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma uliyopo Jijini Dodoma ambapo wajumbe wa Bodi hiyo na Menejimenti ya GST wameshiriki. Aidha, Prof. Ikingura amesisitiza kuhakikisha ukusanyaji wa sampuli za miamba za kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Jiolojia (Geological Museum) unafanyika wakati wa ugani na kuweka mwongozo wa namna bora ya ukusanyaji wa sampuli hizo. Katika hatua nyingine, Prof. Ikingura ameielekeza Menejimenti ya GST kuhakikisha inatangaza kwa Umma matokeo na umuhimu wa tafiti zinazofanywa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuufahamisha Umma. Pamoja na mambo mengine, Prof. ...

Rea yahamasisha wananchi kuchangamkia fursa

Na Mwandishi Wetu  REA;Dar es salaam *WANANCHI WAHAMASISHWA KUCHANGAMKIA FURSA* *📌NI YA UJENZI NA UENDESHAJI WA VITUO VIDOGO VYA BIDHAA ZA MAFUTA VIJIJINI* *📌MKOPO WA HADI SHILINGI MILIONI 133 KUTOLEWA* Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inahamasisha wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo kwa ajili ya Kuwezesha ujenzi na Uendeshaji wa vituo vidogo vya bidhaa za mafuta ya Petroli na Dizeli kwa maeneo ya vijijini. Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya amesema hayo Jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2024 katika Kongamano la 10 la Jotoardhi (ARGeo-C10).  "Hii ni fursa kwa wajasiriamali, makampuni, vikundi ama mtu mmoja mmoja kupata mkopo nafuu na kuwekeza maeneo ya vijijini kwa kujenga na kuendesha kituo cha bidhaa za mafuta ya petroli na dizeli," alisema Mhandisi Yesaya. Mhandisi Yesaya alisema Serikali inatambua maeneo mengi ya vijijini yana uhaba wa mafuta na kwamba wananchi wanatumia madumu kuuzia mafuta ya bidhaa za pet...

Mikataba ya ujenzi wa km 168 za barabara yasainiwa

DAR ES SALAAM Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 24, 2024 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya awali ya ujenzi wa zaidi ya kilomita 168 za barabara za Mkoa wa Dar es Salaam, zitakazojengwa na mradi wa DMDP awamu ya pili. Akizungumza katika hafla hiyo mkoani Dar es Salaam, Mchengerwa amesema jumla ya zabuni 19 tayari zimetangazwa na zipo katika hatua mbalimbali za manunuzi ambapo kati ya zabuni hizo leo umefanyika utiaji saini wa mikataba nane ya awali yenye thamani ya shilingi Bilioni 190.04 inayokwemda kujenga jumla ya kilomita 63.66 za barabara. Mchengerwa amesema kwa mikataba iliyobaki yenye thamani ya shilingi Bilioni 262.46, zitajengwa kilomita 104.56 za barabara ambapo ndani ya mwezi Novemba 2024 itakuwa imekwishasainiwa. Mradi wa DMDP awamu ya pili unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam zikiwemo barabara, masoko, vituo vya mabasi, mifereji ya maji ya mvua, maeneo ya wazi pamoja na...