_▪️Asisitiza Tanzania sio shimo la bidhaa zisizokuwa na ubora_ _▪️Ataka viwanda kuzalisha bidhaa bora zinazouzika ndani na nje ya nchi_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Shirika la Viwango Tanzania kutokuwa na huruma na bidhaa zisizokuwa na ubora kwani Serikali inataka soko la Tanzania liwe na bidhaa bora, salama na zenye kuleta tija kwa mlaji na kwa uchumi. Amewataka wazalishaji wa bidhaa na huduma, wahakikishe wanazingatia taratibu za vipimo, uthibitishaji wa ubora, na uboreshaji wa mifumo ya uzalishaji. “Muhakikishe bidhaa zenu zinakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa vilivyowekwa na TBS”. Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Juni 4, 2025) baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la maabara na ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ambapo amesisitiza kufuatwa kwa viwango vya ubora. Waziri Mkuu ametoa wito kwa wafanyabiashara na waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, wana wajibu wa kuhakikisha bidhaa wanazoing...
Marato tv - Sauti ya Jamii