Skip to main content

Posts

Showing posts from May 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

NBS Yazindua Tafiti za kipekee,Matokeo yake yatoa Taswira ya hali ya wanawake Nchini

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imezindua matokeo ya tafiti mbili muhimu zilizotajwa kuwa miongoni mwa nyenzo zitakazosaidia Taifa kupanga maendeleo kwa kutumia takwimu sahihi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Tafiti hizo ni Utafiti wa Uwezeshwaji Wanawake na Lishe wa Mwaka wa Kilimo 2023/2024 pamoja na Utafiti wa Mazingira na Jinsia wa mwaka 2025, zilizofanywa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Benki ya Dunia, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) na UN Women. Akizindua Tafiti hizo leo Mei 6, 2026 katika Makao Makuu ya ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini Dodoma, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Tafiti hizo zimefungua ukurasa mpya wa matumizi ya takwimu katika kuibua suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii. “Hizi ni tafiti za kwanza kufanyika Tanzania, na kwa upande wa Afrika, utafiti wa mazingira na jinsia ni wa pili baada ya Senegal. Hii ni fahari kubwa kwa Taifa letu,” amesema Dkt. Gwajim...

Dkt.Mwigulu Aelekea Morogoro Kwa Ziara ya Kikazi

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 7, 2026 amesafiri kwa Treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kutoka jijini Dodoma kuelekea Morogoro ambapo kesho Mei 8, 2026 anatarajiwa kuwa na ziara ya kikazi mkoani humo. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameambatana na Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Prof. Palamagamba Kabudi, pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji.

Tanzania: Mahakama Kuu Yafutilia Mbali Maombi ya Benki ya Standard Chartered na Kuitaka Kulipa Gharama

Na Mwandishi wetu Jaji Musa K. Pomo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Biashara Dar es Salaam, ametupilia mbali ombi la Benki ya Standard Chartered kuongezewa muda wa kukata rufaa ya Agosti 26, 2020 iliyotengua hukumu ya Uingereza dhidi ya Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), na kuamua kuwa waombaji walishindwa kupeleka maombi yao ndani ya Muda uliopangwa kisheria. Uamuzi katika Ombi la Kibiashara Nambari 1361 la 2026,  Dar es Salaam na kutolewa uamuzi wake tarehe 5 Mei, 2026, linahitimisha jaribio la Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited na Standard Chartered Bank Malaysia Berhad la kufufua Rufaa Na. 386 ya 2022. Jaji Pomo alisema mahakama zimekuwa zikikosa ulaini kwa washitakiwa wanaoshindwa kufuata amri za mahakama, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwasilisha mawasilisho ya maandishi ndani ya muda uliopangwa. Mhe. Pomo alibainisha: "Nimechunguza maombi na hati yake ya kiapo ya kuunga mkono, hati ya kiapo ya pamoja ya mlalamikiwa wa kwanz...

High Court Commercial Division Dismisses Standard Chartered’s Extension Bid With Costs for ‘Failure to Prosecute’

By Prosper Makene  DAR ES SALAAM – Justice Musa K. Pomo of the High Court of Tanzania, Commercial Division at Dar es Salaam, has dismissed with costs Standard Chartered Bank’s application to extend time to appeal the 26th August 2020 set-aside of its UK judgment against Independent Power Tanzania Limited (IPTL), ruling that the applicants failed to prosecute their application. The ruling in Misc. Commercial Application No. 1361 of 2026, dated at Dar es Salaam and delivered in chamber on this 5th day of May, 2026, ends Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited and Standard Chartered Bank Malaysia Berhad’s attempt to revive Civil Appeal No. 386 of 2022. Justice Pomo held that courts have not been soft with the litigants who fail to comply with court orders, including failure to file written submissions within the time frame ordered. Hon. Pomo noted: "I have given due scrutiny the application and its supporting affidavit, the joint counter affidavit by the 1st and 2nd respondents; ...

Nimeamua kusherehekea Miaka 41 na watoto 41-Faraja Kotta

📍Atimiza miaka 41 na kusherehekea kwa aina ya kipekee 📍Aguswa na uchungu wa kuishi bila wazazi Na MWANDISHI WETU, Muheza NIMEAMUA kuweka alama ya kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa kwa kuamua kuwa mlezi wa watoto 41 wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto hao 41 kama ilivyo miaka aliyoishi duniani, Faraja Kotta mwanasiasa chipukuzi, alisema ameguswa kufanya hivyo kwa sababu maumivu ya kupoteza wazazi akiwa mdogo bado anayahisi hadi leo. Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Mei 6 mwaka huu, katika kituo cha Daarul Abideen, kilichopo Mkanyageni wilayani Muheza Faraja alisema sherehe yake hiyo itabaki katika Kumbukumbu ya maisha yake. Faraja amejitwika jukumu la ulezi kwa watoto hao wanaotoka katika kata 17 za wilaya hiyo, akiahidi kuwasaidia katika huduma za afya kupitia bima, elimu, na mahitaji ya msingi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watakaoguswa kuungana naye katika jukumu hilo. " Niliamua kuweka alama ya kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa kwa kuamua kuwa mlez...

Kikwwte:Rais Samia anaendelea kuwapa tumaini,furaha na Neema watumishi wa Umma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amesema hatua kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan zimeendelea kurejesha matumaini, furaha na ari mpya kwa watumishi wa umma nchini. Kikwete aliyasema hayo wakati akizungumza na Maafisa Tawala pamoja na Maafisa Rasilimaliwatu katika mkutano uliofanyika katika Arusha International Conference Centre jijini Arusha, ambapo aliwataka viongozi hao kutekeleza wajibu wao kwa haki, weledi na kuwathamini watumishi wa umma ili waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi. “Nimewakumbusha kuleta furaha kwa watumishi wa umma ili nao waweze kupeleka furaha na neema kwa Watanzania,” amesema Kikwete. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya maamuzi makubwa yenye kugusa moja kwa moja maisha ya watumishi wa umma, hatua ambazo zimeonesha dhamira ya dhati ya kuboresha ustawi wao pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za seri...

DKT.Mahera Ampongeza Dkt.Samia Kwa mapinduzi ya Elimu ,Ataka fedha za Veta Ziongezwe

MBUNGE wa Jimbo la Butiama, Wilson Charles Mahera ameipongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua kubwa za mageuzi katika sekta ya elimu, akisema uwekezaji unaoendelea unalenga kuifanya Tanzania kuwa taifa la watu wenye ujuzi, ajira na uwezo wa kujitegemea kiuchumi. Akichangia Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Mei 7, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Dkt. Mahera amesema mafanikio yanayoonekana sasa ni mwendelezo wa falsafa ya elimu ya kujitegemea iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Julius Nyerere mwaka 1967, ambayo inalenga kumjenga kijana mwenye ujuzi na mchango wa moja kwa moja kwenye uchumi. Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imeifanyia kazi changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuboresha sera ya elimu na mitaala, hatua inayolenga kuleta elimu yenye uhusiano wa moja kwa moja na soko la ajira. “Kwa uongozi wa Dkt. Samia, tunaona mageuzi ya kweli kwenye elimu. Sasa elimu inazalisha ujuzi, si vyeti pekee,” alisema Dkt. Mahera. ...

Agness Marwa alilia Mara Bungeni,Aitaka Serikali kuwaokoa Walimu Vijijini

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, ameibua kilio cha walimu wanaofundisha katika mazingira magumu vijijini huku akiitaka Serikali kuongeza walimu, kuboresha maslahi yao na kuwapa mazingira bora ya kazi ili kuinua kiwango cha elimu nchini. Akichangia Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Mei 7, 2026 Bungeni Jijini Dodoma, Agnes alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kupitia ajira za walimu pamoja na utoaji wa ufadhili wa masomo ya juu ndani na nje ya nchi. Aidha, ameipongeza Serikali kwa matumizi ya mifumo ya kisasa ya kidijitali ikiwemo School Information System, akisema mfumo huo umeongeza ufanisi katika kufuatilia taarifa za shule, walimu na wanafunzi nchini. Hata hivyo, Agnes amesema bado kuna changamoto kubwa ya uhaba wa walimu katika maeneo mengi ya vijijini, hususan Mkoa wa Mara, jambo linalosababisha walimu wachache kubeba mzigo mkubwa wa wanafunzi. “Walimu wetu wanapitia...

Dkt. Abbasi, Kampuni za Kimataifa Wajadili Mikakati ya Kutangaza Utalii

  Katika kuongeza juhudi za kuitangaza Tanzania kimataifa ili kufikia lengo la watalii milioni 8 mwaka 2030, leo jioni hii Mei 7, 2026, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, katikati ya Mkutano wa Baraza la Utalii na Usafiri Duniani (WTCC), amekutana na kampuni kubwa za kutangaza utalii duniani. Taasisi ya kwanza ni ya Peter Greenberg Worldwide iliyoko California, Marekani, ambapo katika mazungumzo na Mwanzilishi wa kampuni hiyo Bw. Peter Greenberg, viongozi hao wamejadili kuanzia mafanikio ya filamu ya “Tanzania: The Royal Tour,” hadi namna bora ya kuendeleza hatua zijazo za filamu hiyo iliyokonga nyoyo za wengi ndani na nje ya nchi. Aidha, amekutana pia na Bw. Nick Evans, Mwanzilishi wa taasisi ya Beautiful Destinations, yenye ofisi katika miji ya New York, London na Dubai, ikiwa imejikita katika matangazo ya utalii kwa njia za ubunifu, matumizi ya akili-unde na ikijivunia mtandao wa watozi zaidi ya 500 wa maudhui ya kiutalii kutoka maeneo mbalimbali d...

Rais Dkt Samia apandisha madaraja watumishi laki mbili

📍 Apandisha mishahara kwa asilimia 35 Na Mwandishi Wetu, Arusha SERIKALI ya Awamu ya Sita imefanya mageuzi makubwa ya kiutumishi nchini kwa kupandisha madaraja watumishi wa umma 219,042, huku ikiongeza mishahara kwa asilimia 35.1, hatua inayotajwa kuwa ni kielelezo cha uongozi unaoweka mbele ustawi wa mfanyakazi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameyabainisha hayo leo jijini Arusha wakati akizungumza na Maafisa Tawala na Rasilimali Watu katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa AICC. Mhe. Kikwete alisema maamuzi hayo ya kimkakati yaliyopata ridhaa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanalenga kuleta "furaha na neema" kwa watumishi wa umma ili nao waweze kutoa huduma bora na kupeleka furaha kwa Watanzania wote kupitia utendaji wao. Ongezeko la Mishahara na Sekta Binafsi Akifafanua kuhusu neema hiyo ya kiutumishi, Waziri Kikwete alibainisha kuwa mbali na ongezeko la 35.1% kwa watumishi wa umma mwaka 2025, Serikali...

Serikali Yaibuka na Mapinduzi ya Teknolojia ya Nyuklia, Unesco yaipa Tanzania Hadhi Kimataifa

SERIKALI imeendelea kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini baada ya kuanzisha miradi mbalimbali ya matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika kilimo, afya na ufugaji, huku Tanzania ikiendelea kupata heshima kubwa katika majukwaa ya kimataifa kupitia UNESCO. Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma leo Mei 7, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imeanzisha miradi ya kisasa ya nyuklia inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao, kuboresha tiba ya saratani na kuinua sekta ya mifugo. Prof. Mkenda amesema kupitia Tume ya Nguvu ya Atomu Dar es Salaam, Serikali imeanza mradi wa utunzaji wa mazao kwa njia ya mionzi, huku Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) ikiendesha mradi wa kuboresha mbegu ya mpunga kwa teknolojia ya nyuklia ili kukabiliana na ugonjwa wa mabaka ya mpunga na kuongeza uwezo wa mbegu kuvumilia chumvi. Katika sekta ya afya, alisema S...

Serikali yaja na mikakati mipya kuipeleka Elimu Kimataifa

SERIKALI imetangaza mikakati mipya ya kuimarisha sekta ya elimu, sayansi na teknolojia nchini, ikilenga kuongeza ubora wa elimu, kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi pamoja na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha elimu na ubunifu katika ukanda wa Afrika. Mikakati hiyo imetangazwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Mei 7, 2026 Bungeni jijini Dodoma. Prof. Mkenda amesema Serikali imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Umataifishaji wa Elimu wa mwaka 2025 wenye lengo la kuongeza ufanisi katika kuandaa wahitimu wenye maarifa, stadi na umahiri unaokidhi mahitaji ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Amesema mkakati huo pia utaimarisha mitaala na mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuvutia wanafunzi na wanataaluma kutoka nje ya nchi pamoja na kuongeza ushirikiano kati ya taasisi za elimu za ndani na nje ya Tanzania. Katika hatua nyingine, Serikali imeandaa Mkakati wa U...

Serikali yaibuka na Mpango Mkubwa Elimu ya Amali,Vijana 274,000 Kunufaika

SERIKALI imezindua mkakati mpya wa kupanua elimu ya amali na mafunzo ya ufundi nchini huku ikilenga kuwajengea vijana ujuzi wa vitendo utakaowawezesha kujiajiri na kupata ajira katika soko la ndani na kimataifa. Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Mei 7, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda alisema serikali itadahili wanafunzi 374,000 katika vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19 ukilinganisha na mwaka uliopita. “Ongezeko la udahili wa wanafunzi wa vyuo vya ufundi kutaongeza idadi ya vijana wenye ujuzi na uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa,” alisema Prof. Mkenda. Katika kuimarisha sekta hiyo, serikali itasajili vyuo 263 vya elimu ya ufundi, mafunzo ya ufundi stadi pamoja na shule za sekondari za amali, hatua itakayoongeza upatikanaji wa mafunzo ya vitendo kwa vijana wengi zaidi nchini. Prof. Mkenda amesema serikali imeamua ku...