_▪️Wakubaliana kuanzishwa kwa Jukwaa la Wafanyabiashara_ WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire, Robert Beugre Mambe na kujadiliana naye masuala ya kidiplomasia, kiuchumi, teknolojia, kilimo na michezo kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwa mwenyeji wake, Boulevard Angoulvant Plateau, jijini Abidjan. Akitoa ufafanuzi mara baada ya kikao hicho jana jioni (Jumanne, Mei 13, 2025), Waziri Mkuu Majaliwa alisema lengo la kikao chao lilikuwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia lakini pia kuhimiza haja ya nchi hiyo kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ikiwemo utafiti na teknolojia za kisasa kwenye kilimo. “Côte d'Ivoire ina wakazi zaidi ya milioni 31 na inaongoza kwa kilimo cha kakao, korosho na michikichi. Hawa wanalima korosho zaidi kuliko Tanzania, na sisi tunalima korosho kwenye mikoa ya Pwani na kakao kule Mbeya na maeneo mengine. Tunaweza kujifunza kwao na sisi tunaiona hii ni fursa kwetu ya kuongeza uzalishaji kwenye mazao haya.” ...
Marato tv - Sauti ya Jamii