▪️ *Tanzania yaipiku Msumbiji, yaingia 10 bora Afrika* ▪️. *Dhahabu kubadilishwa kwa mafuta, fedha za kigeni* 📍 *Dodoma* WAZIRI wa Madini Mhe. Anthony Mavunde aliweka wazi mafanikio 16 ya Sekta ya Madini katika kipindi cha Miaka Minne ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania kununua Tani 3.7 kwa gharama ya Shilingi 702.3 Bilioni. Akizungumza na Waandishi wa Habari Mei 15, 2025, katika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO), Waziri Mavunde alisema kati ya kiasi kilichonunuliwa takribani, Kilo 2,954 zilisafishwa katika viwanda vya kusafisha dhahabu vilivyoko nchini. Mhe. Mavunde alisema katika Bara la Afrika nchi tano zinazofanya vizuri katika ununuzi wa dhahabu, Tanzania ipo huku nchi ya Algeria ikiongoza. “Miaka mingi nchi yetu iliacha kununua dhahabu kupitia Benki Kuu, lakini mwaka wa fedha 2024/2025 tulifanya marekebisho ya Sheria ya Madini kifungu cha 59 sura ya 123 ambacho kinampa dhamana Waziri wa Madini kujadiliana na wamiliki wa leseni kutenga asilimia ...
Marato tv - Sauti ya Jamii