Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi, Februari 17 Mwaka huu ameshuhudia makabidhiano ya mradi wa uchimbaji wa visima saba vya kilimo cha umwagiliaji katika Mkoa wa Mara na kumtaka mkandarasi wa mradi huo kukamilisha mradi huo kwa wakati. Mhe. Mtambi ametoa maagizo hayo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika kijiji cha Kwikuba, Kata ya Busambara Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na kumtaka mkandarasi huyo na wengine wote ndani ya Mkoa wa Mara kutekeleza miradi yao kwa wakati. “Serikali imekupatia zabuni hii baada ya kujiridhisha na uwezo wa kampuni yenu, sasa Mkoa wa Mara hatutaki visingizio katika utekelezaji wa mradi huu kama kuna changamoto tutaarifiwe mapema ili kuweza kuitatua” amesema Mhe. Mtambi. Mhe. Mtambi anasema miradi ya maendeleo inalenga kutatua changamoto za wananchi na kuwataka wakandarasi wote wa Mkoa wa Mara kujitahidi kukamilisha miradai yao kwa wakati ili iweze kutumika na kutatua kero za wananchi wa Mkoa wa Mara. Kanal...
Marato tv - Sauti ya Jamii