Skip to main content

Posts

Showing posts from December 23, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Rhimo Nyansaho achangia Shilingi Millioni 20 Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ring'wani wilayani Serengeti

 Na Ghati Msamba; Serengeti MKURUGENZI wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania Tanzania, Dk. Rhimo Nyansaho, ametoa mchango wa Shilingi Milioni 20 kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ring’wani kilichopo katika Kata ya Ring’wani, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara. Dk. Nyansaho alikabidhi mchango huo kupitia Mwakilishi wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marco, katika harambee iliyofanyika Desemba 23, 2024, Kijijini Ring’wani. Harambee hiyo ilihusisha wananchi, wadau wa maendeleo, na viongozi wa serikali. Katika harambee hiyo, zaidi ya Shilingi Milioni 84 zilikusanywa, ambapo Dk. Nyansaho alitoa Shilingi Milioni 20 taslimu. Serikali ilitoa ahadi ya Shilingi Milioni 50, na fedha nyingine zilizopatikana ni Shilingi Milioni 6.3 na Shilingi Milioni 8.2 zilizochangwa na Umoja wa Maendeleo wa Ring’wani, na ziliwekwa kwenye akaunti ya ujenzi wa Zahanati hiyo. Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti Angelina  Lubella alieleza kwamba lengo la Serikali ni kuhakikis...

Dkt. Nchemba akaribisha Saudi Arabia Kuwekeza Tanzania

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameikaribisha Saudi Arabia kuwekeza Tanzania katika fursa mbalimbali zikiwemo utalii, kilimo, madini, uendelezaji wa miundombinu pamoja na uchumi wa buluu. Dkt. Nchemba alitoa mwaliko huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchumi na Mipango wa Saudi Arabia, Eng. Ammar Naqadi, Kando ya Mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania, kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Shirika la Kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), lililofanyika hivi karibuni Mjini Riyadh nchini Saudi Arabia. Alibainisha kuwa Tanzania inaendelea na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambapo imeshakamilika kipande kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na ujenzi unaendelea kwa vipande vinavyoelekea Mwanza na DRC kupitia Burundi hivyo ni fursa kwa Saudi Arabia kuwekeza katika miundombinu hiyo ambayo itachochea ukuaji wa bishara kati ya Saudi Arabia, Tanzania na nchi za Afrika Mashariki...

WAZIRI CHANA AMUAPISHA KAMISHNA UHIFADHI NCAA,AMPA MAAGIZO MAZITO

  Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amemuapisha na kumvisha cheo cha kijeshi Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, CC Dkt. Elirehema Joshua Doriye huku akimtaka kuitumia nafasi hiyo kuonesha utendaji uliotukuka na wenye tija kwa maslahi ya Watanzania wote. Hayo yamejiri katika hafla ya kuvishwa cheo na kuapishwa kwa Kamishna Doriye iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro leo Desemba 23,2024. “Ni matumaini yetu makubwa kuwa utaendelea kutumia vipawa vyako kuhakikisha mafanikio makubwa yanapatikana katika mamlaka hii, hususani katika kipindi hiki ambacho sekta ya utalii inaendelea kushamiri duniani. Katika kipindi kifupi cha utendaji wako, tumeona mafanikio makubwa yanayodhihirisha uwezo wako” amesisitiza Mhe. Chana. Aidha, Mhe. Chana amemuelekeza Kamishna Doriye kuhakikisha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inapanua Wigo wa Utalii kwa kuweka mipango ya kuboresha vivutio kama Olduvai Gorge, Mapango ya Amboni, K...

Mbunge Kiswaga atekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo

  Serikali imewaomba wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapindizi (CCM), kwa kukipatia dhamana ya kushika dola katika uchaguzi mkuu ujao, baada ya kutimiza ahadi zake katika maeneo mbalimbali nchini kupitia ilani ya Chama hicho ya mwaka 2020/2025 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, amewasilisha ombi hilo kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Magu, baada ya mbunge wa jimbo hilo Desdery Kiswaga kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho. Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho, mbunge wa jimbo la Magu Desdery Kiswaga, amesema jimbo la Magu katika kutekeleza limepokea shilingi bilioni 143, zilizoelekezwa katika miradi huduma muhimu za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji, barabara Kuhusu miradi ambayo bado haijakamilika, mbunge huyo amesema inaendelea kutekelezwa kwa kasi. Wanachama wa CCM na wananchi, baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama, kwa kauli moja wameridhia tamko la ute...

Benki ya Dunia, Sadc Zampongeza Rais Samia Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

📌 Dkt. Biteko asema nia njema ya Rais Samia iungwe mkono kuleta maendeleo kwa Watanzania 📌 Dkt. Biteko ampongeza Mbunge Kiswaga kwa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo Wilaya ya Magu. Amesema hayo leo Desemba 23, 2024 wilayani Magu mkoani Mwanza katika Mkutano Mkuu Maalum ambapo taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Magu kwa mwaka 2020 hadi 2024 iliwasilishwa. “Mhe. Rais amefanya kazi kubwa ya kupigiwa mfano na anastahili pongezi, nataka niwaambieni kuna watu wengine wanaumia tukimpongeza Rais Samia, lakini wajue hatutoi pongezi hizi peke yetu hata huko duniani kwa mfano Benki ya Dunia na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanampongeza kwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu kwa...

Magu wamshukuru Rais Samia, Dkt. Biteko awahakikishia Maendeleo

📌99% ya vijiji vyafikishiwa umeme magu 📌Majiko ya gesi 3,255 kusambazwa kwa bei ya ruzuku magu. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Ijinga kilichopo kwenye Kisiwa Wilayani Magu Mkoani Mwanza kijiji pekee kilichosalia kufikishiwa umeme wilayani humo kitafikiwa na kwamba zaidi ya shilingi milioni 600 imetengwa na Mkandarasi yupo eneo la mradi. Amesema hayo Wilayani Magu Desemba 23,2024 wakati akihutubia wananchi katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Magu.  "Mnavijiji 82, vijiji 81 vyote vina umeme kimebaki kijiji kimoja kipo kwenye kisiwa na tuliona itachukua muda kuwapelekea umeme kwa kulaza nyaya kwenye maji tukaona watu wa Ijinga ni Watanzania wanastahili kupata umeme tumetenga  milioni 619 ili nao wapate umeme," alisema Mhe. Biteko Alisema Mkandarasi yupo eneo la mradi Kampuni ya Master Volt Ltd yupo kwa ajili ya kupeleka umeme Jua (Solar). Kwa upande wake Mbunge wa Magu, Mhe. Boniventura...