Skip to main content

Posts

Showing posts from September 21, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali yarejesha zaidi ya hekta elfu tatu kwa wakulima wa wilaya Namtumbo

Na NIRC,Namtumbo Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe  ameleta kicheko kwa wananchi wa  kijiji cha Lwinga Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma baada ya kurejesha zaidi ya hekta 3,000 kati ya hekta 6,580 za shamba la serikali kwa wakulima. Waziri Bashe, amesema anatambua kuwa shamba hilo lina  siasa nyingi lakini ni lazima kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya wananchi ambao wana haki ya kumiliki shamba hilo. Akizungumza wilayani humo katika muendelezo wa ziara yake,Waziri Bashe amesema, wananchi wa kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo wana haki ya kumiliki shamba hilo. “Iwapo kuna mwenye hoja awasiliane na mimi haiwezekani wananchi hawa wakose maeneo na wachache watake kujimilikisha wanavyotaka wao"alisema Waziri Bashe na kuongeza kuwa “Shamba hili lilikuwa la wananchi wakalitoa kwa serikali chini ya NAFCO ambao walilitumia kwa miaka nane kisha kulitelekeza  na baadaye kurudishwa wizara ya Kilimo na Kilimo tumelitoa kwa Wakala wa mbegu ASA,limekuwa katika mgogoro kwa zaidi y...

Mkurugenzi Santa Edwin English Medium School kuendelea kusaidia jamii katika sekta ya elimu

  Katika kuhakikisha anaendelea kuingua mkono Serikali kwenye Sekta ya elimu na utoaji wa elimu bora na yenye kuleta tija  kwa watoto wa Kitanzania Mkurugenzi wa Shule ya Santa Edwin English Medium School iliyopo Kata ya Mkolani Jijini Mwanza Bw.Edwin Soko amesema kuwa atahakikisha anaendelea kuisaidia jamii kwa kuendelea kutoa ufadhili wa masomo  kwa wanafunzi kupitia mpango maalumu uliowekwa na uongozi shuleni hapo. Soko ameyasema hayo Septemba.21,2024 katika mahafari ya kwanza ya Darasa la Saba ya shule hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Santa.Edwin ambapo ameongeza kuwa hadi sasa kuna watoto takribani 20 ambao wanapata ufadhili wa masomo shuleni hapo huku lengo kubwa ikiwa ni kurudisha kwa jamii. "Tuna watoto takribani 20 ambao wanapata ufadhili wa elimu bure shuleni kwetu na hii yote ni kurudisha kwa jamii kwani St.Edwin ni jamii"....Alisema  "Ndugu zangu wazazi mbegu hii tunayoipanda hii leo hapa Santa.Edwin English Mediam School naamini ipo siku tutatoa vio...

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ampongeza Rais Samia kusimamia ulinzi na usalama

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutierres kwenye Makuu ya umoja huo na kujadiliana masuala kadhaa yakiwemo ya maendeleo ya jamii, ulinzi na usalama, siasa na ushirikiano wa Tanzania na UN.  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao leo (Jumamosi, Septemba 21, 2024), Waziri Mkuu ambaye yuko Marekani akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79), amesema katika suala la maendeleo ya jamii wamejadiliana umuhimu wa kuinua uwezo wa wananchi kiuchumi ikiwemo upatikanaji wa huduma zote muhimu. Kuhusu ulinzi na usalama, Waziri Mkuu amesema Tanzania imepongezwa kwa kusimamia ukombozi wa nchi nyingi za Afrika hasa za SADC. “Sasa hivi Serikali yetu inaendelea kuunga mkono kwa kupeleka vikosi vya ulinzi kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na za SADC,” amesema.  “Katika hili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amempongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Sul...

Waziri Kikwete ateta na Waziri wa vijana wa smz

 Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Tabia Mwita.  Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar Es Salaam ambapo mkutano wa Vijana na Amani unafanyika.

Majaliwa akutana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 21, 2024 amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres kwenye Ofisi za makao makuu ya umoja huo, New York Nchini Marekani Mheshimiwa Majaliwa yupo nchini humo kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79).

Mchimbaji Chunya auza Dhahabu ya thamani ya shilingi bilioni 20.11

 _Dhana ya Madini ni Maisha na Utajiri Yajibu; *Serikali yapata Mrabaha wa Shilingi Bilioni 1.4* *Shilingi Milioni 402.3 zimelipwa TRA* *Afisa Madini Asema anapaswa kuigwa kwa Uzalendo Aliouonesha kuuzia Sokoni*   Dhana ya Madini ni Maisha na Utajiri imejidhirisha Wilayani Chunya Mkoani Mbeya hivi karibuni baada ya Mchimbaji Mdogo wa Madini ya Dhahabu Aidan Msigwa Septemba 17, 2024 kusajili na kuuza Madini ya Dhahabu katika Soko la Madini Chunya kiasi cha kilo 111.82 zenye thamani ya shilingi bilioni 20.11 Msigwa ni mchimbaji Mdogo wa Madini ya dhahabu katika Wilaya ya Chunya anayemiliki leseni za uchimbaji mdogo (PML) na utafutaji wa madini (PL) katika maeneo tofauti Wilayani Chunya. Aidha, anamiliki mtambo wa uchenjuaji wa madini ya dhahabu wilayani humo. Akizungumza baada ya kufanyika kwa mauzo hayo, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Kimadini Chunya Mhandisi Laurent Mayalla amesema kupitia mauzo hayo, Serikali imepata kiasi cha Shilingi bilioni 1.2 ikiwa ni mrabaha, shiling...

Serikali yaombwa kusapoti juhudi mbalimbali za wadau wa michenzo

Serikali imeombwa kuwaunga mkono wadau mbalimbali wa michezo, wakiwemo JACMA Mining & Service inayofadhili vijana kushiriki mbio za Marathon nchini. Msimamizi wa JACMA Mining & Services JOGGING Club Sylivia Lushokana, amewasilisha ombi hilo, baada ya klabu hiyo kufadhili vijana ishilini kushiriki mbio za Shycom Alumni Marathon, zilizofanyika mkoni Shinyanga. Mratibu wa mbio za Shycom Alumni Marathon Jackson Busilu, ameishukuru kampuni ya Kampuni ya JACMA Minning & Service kwa kushiriki mbio hizo. Mbio za Shycom Alumni Marathon zimewashikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Rais wa Femata atoa siku 6 kufanyika kwa viongozi wapya wa Mkoa wa Geita

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Nchini  (FEMATA), John Bina, ameagiza uongozi wa Mkoa wa Geita kuhakikisha wanatekeleza uchaguzi wa viongozi wapya ndani ya siku sita. Agizo hili limetolewa kutokana na Mkoa wa Geita kuwa wa mwisho katika kuandaa wawakilishi watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa FEMATA unaotarajiwa kufanyika Mkoani Tanga. Bina alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake mkoani Geita iliyolenga kusikiliza na kujadili changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. Alisisitiza umuhimu wa viongozi waliopo kutumia muda uliosalia kuitisha mkutano wa wanachama wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Geita (GEREMA), ili kufanya uchaguzi wa viongozi wapya. Kwa upande wao, baadhi ya wanachama wa GEREMA, wakiwemo Misana Nyabange na Godfrey Miti, wameelezea hitaji la kuharakisha mchakato wa uchaguzi ili kuanza maandalizi ya uchaguzi katika ngazi za wilaya na matawi mengine ya wachimbaji wadogo. Uchaguzi huu unatajwa kuwa muhimu kwa kuhakikisha ...