Skip to main content

Posts

Showing posts from October 17, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko na waziri wa nyumba Misri kusimamia ukamilishaji mradi wa Jnhpp

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Oktoba 17, 2024 jijini Dar es salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nyumba, Huduma na Jumuiya za Mijini kutoka nchini  Misri, Mhe. Sherif EI Sherbiny. Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kusimamia wakandarasi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kukamilisha mradi huo kwa wakati ambao hadi sasa umefikia asilimia 99 ya utekelezaji wake. Aidha, Mhe.  EI Sherbiny ambaye ameteuliwa hivi karibuni katika nafasi hiyo akiwa nchini  atataembelea mradi wa JNHPP.

Serikali kuwezesha vifaa vya uongezaji thamani madini ya vito na usonara kwa vijana wahitimu wa kituo cha Jimolojia(Tgc)

●Ni utekelezaji wa Programu ya Mining For a Brighter Tomorrow(MBT) ⚫️Wizara ya Madini kuwapatia  vifaa kwa lengo la kujiajiri ●Kuwajengea Uwezo wa masoko na kuwaunganisha na sekta ya ajira ●Lengo ni kuendeleza Ujuzi wa kiufundi na Ubunifu kwenye uongezaji thamani madini *Dodoma*  Imeelezwa kwamba Wizara ya Madini kupitia Mpango wa Uchimbaji Madini wa Kesho yenye matumaini (MBT) kwa vijana watakaohitimu katika Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC)  kuwawezesha kwa kuwapatia vifaa na mashine za Uchongaji, Ukataji na Usafishaji madini ghafi zitakazo pelekea kuwa bidhaa bora zenye thamani ya juu. Hayo yameelezwa leo Oktoba 16, 2024 na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde wakati akitoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma. Waziri Mavunde amesema kuwa, Kituo cha TGC kinatoa mafunzo  kupitia vifaa vya kisasa hususan katika uongezaji thamani madini ya vito kwa Ukataji Uchongaji na Usafishaji, hivyo kwa Mwaka wa Fed...

Mwili wa Mbuge wazikwa kijeshi kwa kupigwa mizinga kumi na mitatu

Hatimaye Mwili wa meja Jenerali mstaafu wa jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania Chalres Mbuge umezikwa kwa heshima zote za kijeshi kijijini kwake. Mwili  wa afisa huyo wa ngazi ya juu wa JWTZ  umezikwa leo Oktoba 17 2024 majira ya saa sita na dakika 13 katika kitongoji cha Nyamongo,kijiji cha Kiabakari wilayani Butiama mkoani Mara. Mazishi hayo yaliongozwa na kanisa katoliki kabla ya kufanyika kijeshi yameshuhudiwa na mkuu wa majeshi mstaafu jenerali VENACE MABEYO,wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu wakiongozwa na mkuubwa mkoa wa Mara kanali Evans Mtambi. Maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la wananchi wameongozwa mkuu wa jeshi la kujenga  Taifa (JKT)  meje jenerali Rajab Mabele akimwakilisha mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini jenerali JACOBO JOHN MKUNDA.  Akizungumza kabla ya mazishi hayo,meja Jenerali Mabele mbali na kumuelezea marehemu enzi za uhai wake jinsi alivyokuwa mshauri katika majukumu mbali mbali ya kikazi amesema Taifa limepata pigo kwa kulndokewa na meja...

Waziri mkuu amesema Tanzania yajiandaa kurusha satelaiti chini ya umoja wa mataifa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza wa Mpango mkakati wa miaka mitano 2024/25 – 2029/30 wa Anga za juu utakaoiwezesha Tanzania kurusha satelaiti. Amesema kuwa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam imepata mradi wa Utafiti wa kuwezesha urushaji wa satelaiti unaosimamiwa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya anga za juu ikishirikiana na Taasisi ya Anga za Juu ya Japan (JAXA). Amesema hayo leo (Alhamisi Oktoba 17, 2024) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA, lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.   “Katika eneo hili Maandalizi ya utungwaji wa Sera, Sheria na uridhiwaji wa mikataba ya Kimataifa ya masuala ya anga za juu inaendelea”. Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iwakusanye vijana wabunifu wenye uwezo wa kubuni teknolojia zenye manufaa kwa Taifa “Lakini simamieni hizi tafiti zenye ku...

Mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge wazikwa kijijini kwake Kiabakari wilayani Butiama Mkoani Mara

  Mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge umezikwa katika kijiji cha kiabakari kitongoji cha Nyamongo wilayani Butiama Mkoani Mara.  Maafisa wa ngazi ya Juu wa JWTZ,Viongozi wa serikali na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo WAKISHUHUDIA MWILI wa Jenerali Mstaafu Mbuge ukishushwa kaburini Oktoba 17 kijijini kwake Kiabakari. 

Majaliwa amwakilisha Rais Dkt.Samia kilele kongamano la Tehama

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 17, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA, linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. Akizungumza baada ya kutembelea mabanda  ya Maonesho kwenye Kongamano hilo, Mheshimiwa Majaliwa  ameipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanasimamia ukuaji wa Sekta ya TEHAMA. Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amewataka vijana kutumia fursa ya Uwekezaji unaofanya na Serikali katika sekta ya TEHAMA ili kukuza uchimi binafsi na Taifa kwa ujumla Kaulimbinu ya Kongamano hilo ni “Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Robotiki kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii".