Mbunge Mavunde Akabidhi Matofali 41,000 na Saruji Tani 102 Kuchochea Shughuli Za Maendeleo Dodoma Jiji
▪️Ni kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi kwa kata zote 41 ▪️Jiji la Dodoma latenga Bilioni 6 kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi ▪️Vifaa kulenga kuboresha sekta ya Afya na Elimu ▪️Rais Samia apongezwa kwa maendeleo makubwa Dodoma Jiji Mwenyekiti wa kamati ya Mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amekabidhi matofali 41,000 na Saruji tani 102 kwa kata zote 41 za Dodoma Mjini kwa lengo la kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya Elimu na vituo vya Afya. “Mfuko wa Jimbo hujielekeza katika miradi ya kipaumbele ya Elimu,Afya na uwezeshwaji wananchi kiuchumi. Leo tunakabidhi matofali na saruji kwa kata zote 41 kwa lengo la kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi. Kwasasa Jiji la Dodoma limetenga Shilingi Bilioni 6 kuunga mkono miradi yote inayoibuliwa na wananchi ili kuchochea maendeleo zaidi ndani ya Dodoma Jiji. Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan amefanya kazi kubwa sana ya kuiendeleza Do...