Skip to main content

Posts

Showing posts from November 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 26, 2025 anafungua Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini Mwaka 2025 yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Malengo ya maadhimisho hayo ni pamoja na kuimarisha usalama na ufikivu wa huduma za usafiri wa nchi kavu kwa kukuza mifumo salama, jumuishi na endelevu ya usafiri wa ardhini kwa njia ya barabara na reli  Pia, yanalenga kukuza ushindani wa haki na ubora wa huduma katika usafiri wa nchi kavu kwa kuhakikisha waendeshaji wanatoa huduma za bei nafuu, zenye uhakika na ubunifu chini ya mfumo madhubuti wa udhibiti wa LATRA. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni *“Nishati Safi na Ubunifukatika Usafirishaji.”*

Serikali Yawahakikishia Wananchi Umeme wa Uhakika

📌Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba atembelea Kituo cha Zuzu Dodoma 📌Asisitiza umuhimu wa utunzaji na ulinzi wa miundombinu ya umeme na vituo vya kupoza na kusambaza umeme Na Mwandishi Wetu, Dodoma Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba amesema, Serikali inawahakikishia wananchi upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuwataka wananchi wa Dodoma na wadau mbalimbali kuwekeza katika shughuli za kiuchumi zinazohitaji umeme bila ya shaka yoyote kwani umeme upo wa kutosha na wa uhakika. Naibu Waziri Salome Makamba ameyasema hayo leo tarehe 25 Novemba, 2025 mara baada ya kutembelea Kituo cha Kupokea, Kupoza  na Kusambaza umeme cha Zuzu kilichopo Jijini Dodoma na kueleza kuridhishwa kwake na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa mafanikio makubwa katika Kituo hicho. Ameeleza kuwa wakati kituo hicho kinaanzishwa mwaka 1986 mahitaji ya umeme katika Kituo hicho yalikuwa MW 2 .5 tu lakini kwa sasa mahitaji ya umeme kwa Mkoa wa Dodoma ni MW 86. “Serikali ya awamu ya sita inaen...

Tawa Yagusa Maisha ya Wananchi Meatu

📍Yajenga Zahanati, Madarasa na Ofisi za walimu  📍Kauli Mbiu ya "Kazi na Utu" Yaanza Kutekelezwa Kwa Vitendo na Kishindo  Na Beatus Maganja, Meatu  Wananchi wa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wanatarajiwa kuondokana na adha ya upatikanaji wa huduma za afya na elimu baada ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kwa kushirikiana na Kampuni ya Kitalii ya Mwiba Holdings Ltd. kuibua miradi ya ujenzi wa zahanati moja katika Kijiji cha Matale,  madarasa manne  na ofisi mbili za walimu katika Kijiji cha Mbughayabanyha. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia TAWA na wadau wake  katika kutatua changamoto za wananchi na kuhakikisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi zinanufaika moja kwa moja na rasilimali za wanyamapori. Akizungumza katika hafla ya  uwekaji jiwe la msingi katika miradi hiyo Novemba 25, 2025 iliyofanyika katika vijiji hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe. Fauzia  Ngatumbura aliipongeza TAWA Kwa kushirikiana na Kamp...

Makamu wa Rais Ashiriki Mkutano wa Siku Mbili wa AU-EU Nchini Angola

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameshiriki Mkutano wa 7 wa Viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya (AU-EU Summit), uliofanyika  Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 25 Novemba 2025. Mkutano huo uliofanyika kwa Siku mbili, pamoja na mambo mengine umehitimishwa kwa dhamira ya kuunda mustakabali mwema na endelevu wa Afrika na Ulaya, ushirikiano mpya na imara juu ya amani, usalama na utawala katika kukabiliana na vita na migogoro kote ulimwenguni. Masuala mengine yaliyopewa kipaumbele katika Mkutano huo ni pamoja na ahadi madhubuti ya ushirikiano wa kimataifa pamoja na ushirikiano imara na wa kuheshimiana katika masuala ya uhamiaji na uhamaji. Mkutano huo pia umedhamiria kuendelea kusaidia nchi zote za Kiafrika katika maendeleo, viwanda, kuongeza mauzo ya nje, na kuunganisha katika masoko ya kikanda. Pia makubaliano yamefanyika katika nia ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA). Pia k...

SERIKALI YAFUTA LESENI 73 ZA WACHIMBAJI WA MADINI

▪️Ni Leseni za Utafiti na Uchimbaji Madini wa Kati. ▪️Ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia  kuwezesha Vijana  *■ Waziri Mavunde aelekeza zielekezwe kwenye Programu ya MBT na wawekezaji walio tayari *■ Eneo la ekari 741,494 lilihodhiwa bila kufanyiwa kazi *DODOMA* WAZIRI wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde ameilekeza Tume ya Madini kufuta leseni 73 za uchimbaji wa kati na utafiti wa madini ambazo hazijaendelezwa. Mhe. Mavunde ametoa maelekezo hayo leo Novemba 25, 2025 wakati akiongea na vyombo ya habari katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Madini mjini Dodoma. Mhe. Mavunde amesema kuwa , ufutaji wa leseni hizo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuiwezesha Wizara ya Madini kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa na kuhakikisha rasilimali  madini zinawanufaishaWatanzania na Taifa kwa ujumla. Mhe. Mavunde ameongeza kuwa, eneo lenye ukubwa wa ekari 741,494 lilihodhiwa ...

Wafanyabiashara wa Madini Waendelea Kuleta Madini yao

Kuelekea Mnada wa Tatu wa Madini ya Vito Jijini Arusha_ 📍*Arusha* Wafanyabiashara wa madini nchini wameendelea kuwasilisha madini mbalimbali katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kama sehemu ya maandalizi ya kuelekea mnada wa tatu wa madini ya vito unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha mnamo Alhamisi, Novemba 27, 2025. Hatua hii inalenga kuhakikisha madini yote yanayokusudiwa kuuzwa yanachambuliwa na kuthaminishwa kabla ya kuingizwa kwenye mnada, hatua inayoongeza uwazi na kuimarisha thamani ya madini nchini. Mnada huo unatarajiwa kuvutia wanunuzi wa ndani, hivyo kuongeza fursa na ushindani kwa wafanyabiashara hivyo kuongeza ukuaji wa sekta ya madini.