Skip to main content

Posts

Showing posts from April 29, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Chana akutana na Sekretarieti ya mkataba wa Lusaka

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya mkataba wa Lusaka (Lusaka Agreement) kuhusu Mkutano wa 14 wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka(LATF) unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Mei 6-8, 2025. Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma leo Aprili, 30 2025 Mhe. Chana amesema Tanzania iko tayari kupokea  wageni zaidi ya 100 kutoka Nchi wanachama na Nchi waalikwa na kuwahakikishia usalama wao kwa kipindi chote wawapo nchini.  Naye, Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Mkataba wa Lusaka, Bw. Edward Phiri amesema maandalizi  ya mkutano huo yamekamilika  na  tayari viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Mkataba wa Lusaka wameshathibitisha kushiriki. Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia maliasili), CP Benedict Wakulyamba , Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili...

Waziri Kabudi afurahishwa na mjasiliamali aliyenufaika na mfuko wa SDF

  Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka watanzania wasiogope kuwa wajasiriamali wa kilimo kwani kinalipa. Amesema hata kilimo cha uyoga kimewanufaisha wajasiriamali wengi akiwemo Esther Shebe ambaye amenufaika na mafunzo ya kuendeleza ujuzi kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Ameyasema hayo leo wakati alipotembelea TEA kwenye hafla ya kufunga maonyesho ya kitaifa ya kazi za utamaduni na Sanaa yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Akiwa kwenye banda hilo baada ya kusikiliza mafanikio ya mjasiriamali huyo, Waziri Kabudi aliwataka watanzania wasiogope kufanya ujasiriamali wa Kilimo kwani wanaweza kunufaika kama Shebe ambaye amemudu kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na Uyoga. “Nimefurahi sana kuona namna ulivyoweza kutengeneza bidhaa nyingi kwa kutumia uyoga nahamasiha na wengine wafanye kama wewe wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali akishiriki kikao cha Bunge Jijini Dodoma Aprili 30 - 2025

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel M. Maneno na Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius J. Njole wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa  Mkutano wa Kumi na Tisa, Kikao cha Kumi na Tano cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria inatarajiwa kuwasilishwa katika Kikao hicho cha Bunge leo tarehe 30 Aprili, 2025. #BajetiyaWizarayaKatibanaSheria

Tija kwa Nchi ndiyo kipaumbele cha utekelezaji wa mradi wa kuchakata gesi asilia ( LNG ) - DKT Biteko

  📌 *Asema kiu ya Serikali ni kuona mradi unatekelezwa ila maslahi ya Taifa ndiyo kipaumbele* 📌 *Alieleza Bunge hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhamasisha ujenzi wa vituo vya gesi (CNG) na matumizi* 📌 *Aeleza kuhusu kuundwa kwa Timu kuangalia unafuu wa gharama za umeme kwa Wananchi* 📌 *Kapinga azungumzia kazi za kupeleka umeme wa Gridi Rukwa, Kagera, Katavi, Lindi na Mtwara* 📌 *Shilingi Bilioni 9.89 kupeleka umeme jua kwenye visiwa 118* 📌 *Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati 2025/2026 kwa asilimia 100* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko amesema dhamira ya Serikali ni kutekeleza mradi mkubwa wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) kutokana na faida zake kiuchumi ila kwa sasa kuna maeneo ambayo Serikali inayafanyia kazi kwa kina kupitia majadiliano na Wawekezaji ili mradi husika uwe na tija kwa nchi na wananchi. Ameyasema hayo tarehe 29 Aprili 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na Wabunge kuhusu Hotuba...

Zuieni mianya inayoashiria upotevu wa fedha - Dkt Mfaume

  OR-TAMISEMI Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume  ameuelekeza uongozi wa kituo cha afya cha Buguruni *kudhibiti* mianya ya upotevu wa fedha katika kituo hicho ili kuendelea kuboresha miundombinu ya kituo na kufanikisha utoaji wa huduma kwa *wananchi* . Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo mara baada ya kutembelea na kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika kituo cha afya cha Mnazi Mmoja na kituo cha afya cha Buguruni. “ *Tunapolenga* upatikanaji wa huduma za afya kwa ubora zaidi lazima *tudhibiti* mianya ya upotevu wa fedha na *kuongeza* mapato *kwa* kutoa huduma bora Kwa wateja wetu” amesisitiza Aidha, Dkt. Mfaume ametaka timu ya *Usimamizi* wa *Huduma* za Afya (CHMT)  katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam *kuongeza* usimamizi wa fedha katika kituo vituo mbalimbali katika Halmashauri hiyo. Pia Dkt. Mfaume ameielekeza timu ya Usimamizi wa *Huduma* za Afya (CHMT) kushirikishana n...

Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya.

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amehitimisha mafunzo ya Askari wapya katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi iliyopo Kihangaiko, Msata Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, leo tarehe 29 Aprili 2025. Askari waliohitimu mafunzo wamekula kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.  Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Mkunda amewataka Askari wapya kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kiapo cha utii, na kuwajibika kulinda mipaka ya nchi, kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Askari wapya wametakiwa kutunza afya zao kwa kuwa muda wote wanatakiwa kuwa na utimamu wa afya ili waweze kulitumikia Taifa kama walivyokusudiwa. . Aidha, Jenerali Mkunda amewaasa Askari kuzingatia mambo manne kwa Mwanajeshi ambayo ni Nidhamu nzuri, Utii, Uhodari na Uaminifu kwani Taifa linawaamini na kuwategemea katika ulinzi.

Wabunge wampongeza Dkt.Biteko Bajeti kupita kwa kishindo

  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakipongezwa na Wabunge mbalimbali mara baada ya Bunge kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2025/2026. #IMEPITA #BAJETI2025/2026

Mnufaika uhitimu masomo,lipa mkopo wako kwa wakati

  Na Dk. Reubeni Lumbagala  SERIKALI kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawajibika kupokea maombi ya mikopo na kutoa mikopo kwa waombaji waliokidhi vigezo vilivyowekwa. Bodi ya Mikopo ambayo sasa imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004, hadi Februari 2025, HESLB inajivunia kutoa takribani shilingi trilioni 8.2 kwa waombaji mbalimbali zaidi ya 830,000 ambao sasa si waombaji tena bali ni wanufaika wa mikopo hiyo.  Kiukweli, fedha hizi ni nyingi sana ambazo zimetolewa na serikali kwa nia njema ya kuwasaidia wanafunzi ambao kutokana na hali za kiuchumi wao na familia zao hawawezi kugharamia gharama za elimu ya juu, hivyo kuhitaji kuwezeshwa raslimalifedha ili kumudu kulipa ada, malazi, kununua chakula, vitabu, kuhudhuria mafunzo kwa vitendo na masuala mengineyo. Ni muhimu kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kufahamu kuwa mikopo waliyokopeshwa na serikali kupitia Bodi ya Mikopo inapaswa kurejeshwa pindi wanapohitimu masomo yao hasa ba...