Skip to main content

Posts

Showing posts from February 4, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kairuki: Sekta ya Mawasiliano yapiga hatua kubwa Ndani ya Siku 100 za Uongozi wa Awamu ya Pili ya Rais Samia

KAIRUKI: SEKTA YA MAWASILIANO YAPIGA HATUA KUBWA NDANI YA SIKU 100 ZA UONGOZI WA AWAMU YA PILI YA RAIS SAMIA. Na  Mwandishi wetu Dodoma  Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Angela Kairuki, amesema Sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeendelea kukua kwa kasi kubwa ndani ya siku 100 za utekelezaji wa kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri Kairuki alisema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo minara ya simu na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. “Takwimu zinaonesha kuwa laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 99.3 mwezi Oktoba 2025 hadi kufikia milioni 106.9 Januari 2026, sawa na ongezeko la asilimia 7.7,” alisema Waziri Kairuki. Aliongeza kuwa idadi ya watumiaji wa intaneti imeongezeka kutoka milioni 56.3 hadi milioni 58.1 kati...

Sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Yaendelea Kuchangia Kasi ya Ukuaji wa Uchumi Nchini-Waziri Kairuki

 DODOMA. KATIKA kipindi cha siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeendelea kukua kwa kasi ikichangiwa na uwekezaji ulioendelea kufanywa na Serikali hususani kwenye ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano ikiwemo Minara na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Akielezea amafanikio hayo ya siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani Leo Feb 4,2026, waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Angel Kairuki amesema upatikanaji wa Mawasiliano nchini unaendelea kuimarika. Amesema mwenendo huo unaashiria kuendelea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano na teknolojia ya habari katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za mawasiliano.  "Takwimu zinaonesha kuwa laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 99.3 Oktoba, 2025 hadi laini milioni 106.9 Januari, 2026 sawa na ongezeko la asilimia 7.7". Amesema "Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 56.3 Oktoba, 2025 hadi milioni 58.1 Januari, 2026 saw...

Waziri Mkuu Afanya Mazungumzo ya Kimkakati na Viongozi Waandamizi wa Serikali na Wadau

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi ya Usafirishaji wa Bima ya Mikopo (KUKE) kutoka nchini Poland ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma leo Februari 4, 2026. Viongozi hao wamejadili kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR kipande cha 3 na 4) pamoja na kujadili fursa za kuimarisha ushirikiano wa kifedha baina ya Tanzania na Serikali ya Poland.

Hospitali ya Shifaa Kinondoni Yasema Sarani Inatibika Ukiiwahi

Na Mwandishi Wetu WATANZANIA wametakiwa kuondokana na dhana kwamba saratani haitibiki na badala yake wawahi hospitalini kupima kila wanapoona dalili mbaya kwani saratani inatibika kama mgonjwa atawahi kupima mapema na kuibaini. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salam na Daktari bingwa wa saratani wa hospitali ya Shifaa iliyoko Kinondoni, Barabara ya Msese, Magreth Moshi, wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya saratani duniani. Alisema saratani inaweza kutibiwa kama mgonjwa atakuwa na kawaida ya kupima na kugundulika ikiwa katika hatua ya awali badala ya kusubiri mpaka hali inapokuwa mbaya ndipo waende hospitalini. Alisema kila tarehe 4 ya mwezi wa pili dunia huadhimisha siku ya saratani duniani ambapo elimu hutolewa kwa wananchi kuwahi hospitalini mapema wanapoona dalili mbaya mwilini kama uvimbe usiokuwa wa kawaida. Alisema utambuzi wa mapema wa ugonjwa wa saratani unatoa ahueni kwa mgonjwa kwani uwezekano wa kupona unakuwa mkubwa zaidi kuliko akichelewa kwenda kufanya vipim...

Waziri Mkuu Afanya Mazungumzo ya Kimkakati na Viongozi Waandamizi wa Serikali na Wadau

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi ya Usafirishaji wa Bima ya Mikopo (KUKE) kutoka nchini Poland ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma leo Februari 4, 2026. Viongozi hao wamejadili kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR kipande cha 3 na 4) pamoja na kujadili fursa za kuimarisha ushirikiano wa kifedha baina ya Tanzania na Serikali ya Poland.

Dc Itunda Apongeza Jitihada Za Rais Samia Mageuzi ya Kidigitali Mahakamani

📍Azindua wiki ya Sheria Mbeya  *NA MWANDISHI WETU, MBEYA* Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utashi wake wa kisiasa na uwekezaji mkubwa uliowezesha mapinduzi ya kidijitali ndani ya Muhimili wa Mahakama, hatua inayorahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi. Mhe. Itunda ametoa pongezi hizo wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa, katika uzinduzi wa Wiki ya Sheria mkoani hapa. Alisema kuwa uboreshaji wa miundombinu na mifumo ya kisasa ya TEHAMA ni matokeo ya fedha nyingi ambazo Rais Samia amekuwa akizielekeza mahakamani ili kuleta ufanisi, uwazi na uwajibikaji. Akielezea ufanisi huo, Mhe. Itunda amebainisha kuwa kupitia utekelezaji wa maono ya Rais Samia, Mahakama imeweza kuongeza kasi ya kusikiliza na kumaliza mashauri kwa wakati, jambo linalopunguza kero kwa wananchi na kuimarisha utawala wa sheria nchini. "Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuipa ki...

Wizara ya Uchukuzi Kuchukua Hatua Kali Kuwalinda Wanafunzi

 DODOMA. WAZIRI wa Uchukuzi Mhe. Prof Makame Mbarawa amekemea vikali vitendo vya baadhi ya madereva na makondakta kukiuka kanuni na taratibu kwa kushindwa kuwabeba wanafunzi wakati wakienda shule na kurejea majumbani kwa madai ya kibiashara,jambo ambalo limesababisha baadhi ya wanafunzi kukatisha Masomo. Waziri Mbarawa amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali na stahiki dhidi ya watu wote wanaokiuka taratibu na kanuni za usafiri, bila kujali nafasi zao. Kauli hiyo ya Serikali imetokana na kuona moja ya picha ya video kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani Jijini Dar es Salam Mariana Eric Mirindima akiwasilisha barua iliyobainisha vitendo vya baadhi ya madereva na makondakta kuwanyanyasa na kuwanyima wanafunzi usafiri kwa madai ya kibiashara.  Barua hiyo imeeleza kwamba kunyimwa usafiri Kwa wanafunzi kunasababisha kuchelewa au kushindwa kufika shuleni, kuhatarisha usalama wao na kuathiri haki yao ya msingi ya kupata elimu. Kat...