Skip to main content

Posts

Showing posts from September 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kamishna wa Uhifadhi Mstaafu Mabula Misungwi Nyanda Aagwa Rasmi Tawa

Na. Joyce Ndunguru, Morogoro. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imemuaga rasmi aliyekuwa Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi Nyanda baada ya kumaliza safari yake ya utumishi wa umma. Akizungumza katika hafla hiyo ya Kijeshi iliyofanyika Septemba 19, 2025, katika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Mej.Jen (Mstaafu) Hamis Semfuko alimpongeza Kamishna Nyanda kwa kuhitimisha safari yake ya utumishi na kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa kwanza wa TAWA aliyedumu kwa muda mrefu na kustaafu akiwa kwenye cheo hiko cha juu katika uongozi wa TAWA. “Kwa namna ya kipekee ningependa kukupongeza na kukushukuru Kamishna Mstaafu Nyanda kwa utumishi wako katika tasnia hii ya uhifadhi na hususan ukiwa kama Kamishna wa TAWA,” alisema Mej. Jen (Mstaafu) Semfuko. Sambamba na hilo, Semfuko aliongeza kuwa chini ya uongozi wa Kamishna Mstaafu Nyanda, TAWA imepata mafanikio mengi yakiwemo kuboresha maslahi ya watumishi, ujenzi...

Eu Yatoa Tahadhari Kuhusu Kupungua Kwa Barafu Mlima Kilimanjaro

Na. Mwandishi wetu - Kilimanjaro. Umoja wa Ulaya (EU) umetahadharisha kuhusu kasi ya kupungua kwa barafu katika Mlima Kilimanjaro, hatua inayotajwa kuathiri kwa kiasi kikubwa mazingira na maisha ya jamii zinazotegemea rasilimali za mlima huo. Akizungumza jana Septemba 19, 2025 wakati wa ziara ya Waheshimiwa mabalozi wa Umoja wa Ulaya waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Balozi wa Finland Nchini Tanzania. Mhe. Theresa Zitting amesema hali ya kuyeyuka kwa barafu katika kilele cha Uhuru ni ishara ya wazi ya mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba dunia. “Ni jambo la kusikitisha kusikia na kushuhudia jinsi barafu inavyopungua na namna hali hiyo inavyotarajiwa kuathiri mtiririko wa maji na mfumo wa ikolojia katika maeneo ya chini ya mlima. Tatizo hili halipo Tanzania pekee; hata nchini mwangu Finland tunashuhudia mabadiliko ya joto,” alisema. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, takribani watalii 60,000 hutembelea  Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kila mwaka, wengi wao ni kutoka nchi ...

Mgombea Ubunge Wa Act Jimbo La Kawe Aongoza Kikosi Kazi Kuzisaka Kura Majumbani

 Matukio katika Picha.  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Bi *Glory Tausi Shayo,* akiongozana na wagombea Udiwani wa Kata ya Kunduchi, Kata ya Kawe, Kata ya Bunju na, Kata ya Mbezi Juu. Wameendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba katika kata ya Kunduchi.  Walifanikiwa kutembelea wafanyabiashara wa Tegeta kwa Ndevu na Kuendelea na Kampeni za Nyumba kwa nyumba, katika mtaa wa Tegeta, Kata ya Kunduchi, Jimbo la Kawe. Team hii ilipata fursa ya kusikia changamoto nyingi, zinazowakabili wafanyabiashara na wananchi wa eneo hili na wameahidi kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.