Skip to main content

Posts

Showing posts from June 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Misa Tan na Ewura yawajengea Uwezo Waandishi wa Habari Kuifahamu Ewura na Majukumu Yake

Mwandishi wetu ;Dar es salaam Semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na majukumu yake inaendelea leo katika ukumbi wa mikutano wa Beachcomber Hotel, jijini Dar es Salaam. Semina hiyo imefunguliwa rasmi na Nyirabu Musira kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, ambapo amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuelewa kazi na majukumu ya EWURA ili waweze kuhabarisha jamii kwa usahihi na ufasaha. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa hiyo  hiyo, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari nchini. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao ni wanachama wa MISA-TAN kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Pwani, Dar es Salaam na Shinyanga, wameahidi kuzingatia yale wanayojifunza kupitia mawasilisho mbalimbali na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo...

Mapokezi ya Rais Samia Mkoa wa Simiyu Usipime

  Maelfu Ya Wananchi Mkoa Wa Simiyu Wajitokeza Kumpokezi Ya Rais Samia

*Balozi Nchimbi: Fidia Mifugo Iliyotaifishwa ihitimishwe

_Asema ni muhimu kutekeleza maamuzi ya mahakama_ _Kampeni ya ‘Tutunzane’ itumike pia kwenye siasa_ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa maelekezo kwa Serikali, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, kuratibu mazungumzo ya kuwalipa fidia wafugaji ambao mifugo yao ilitaifishwa lakini walishinda kesi mahakamani, ili suala hilo limalizike. Balozi Nchimbi amesema kuwa madai ya wafugaji hao, ambao walishinda kesi mahakamani baada ya mifugo yao kutaifishwa kwa tuhuma za kuingiza mifugo maeneo ya hifadhi kinyume cha sheria, yamechukua muda mrefu na yanapaswa kuhitimishwa kwa kutekeleza maamuzi ya mahakama. Dkt. Nchimbi ameyasema hayo wakati akifunga Kongamano la Wafugaji, mkoani Simiyu, katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi, leo Jumapili, tarehe 15 Juni 2024, ambapo pia alisisitiza kuwa dhamira ya CCM ya kuboresha sekta ya mifugo na kubadilisha maisha ya wafugaji haitayumba wala kutetereka, kwani chama kinatambua mchango wao katika uchumi wa taifa. “Kweny...

Balozi Nchimbi Afunga Kongamano la Wafugaji

Matukio mbalimbali katika picha, yakionesha kongamano la wafugaji lililofanyika mkoani Simiyu, Wilaya ya Bariadi, katika viwanja vya Nyakabindi, ambapo mgeni rasmi, aliyelifunga leo Jumapili, tarehe 15 June 2025, alikuwa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.

Ruto:Siwezi Kuachia Mamlaka Kiongozi Yeyote aliye Upinzani Kwa Sasa

RAIS wa Kenya Dokta William Ruto ameapa kutokabidhi mamlaka kwa kiongozi yeyote aliye upinzani kwa sasa akisema wote wamechanganyikiwa na hawana ajenga kwa nchi. Rais Ruto amesema Upinzani wanatafuta kitu kimoja tu, yaani kumwondoa mamlakani bila mipango yoyote mahsusi kwa manufaa ya Wakenya na maendeleo kwa nchi. “Nimeona ajenda yao kuu ni ‘Ruto must go’. Hakuna kingine. Sasa, ‘Ruto must go’ itasaidiaje Wakenya wanaokumbwa na changamoto za matibabu, elimu na matatizo mengine?” alihoji Rais Ruto alipohudhuria ibada ya kanisa katika Shule ya Kivaywa eneo bunge la Lugari, Kaunti ya Kakamega. 

Ukomo wa Madiwani Wote Nchini June 20-2025-Mchengerwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ametanga kuwa Mabaraza yote ya Halmashauri yanapaswa kuvunjwa ifikapo Tarehe 20/06/2025. Ukomo wa Kamati zote za Halmashauri zinazoundwa na Madiwani utakuwa ni Tarehe 20/06/2025. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika atakuwa ndiye Mwenyekiti wa mpito wa Halmashauri akisaidiwa na Wakuu wa Idara kama sehemu ya Kamati hadi hapo Uchaguzi utakapofanyika. Kwa taarifa hii hakuna Diwani atakayeendelea na majukumu yake mara baada ya Tarehe 20/06/2026!

Rais Samia Amuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2025. Matukio mbalimbali kwenye hafla ya uapisho wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Jaji George Mcheche Masaju, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kumuapisha Mhe. Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2025.