*Afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Wilaya Nachingwea WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewaonya watendaji na watumishi wa umma waache tabia ya kuzoea matatizo hasa katika sehemu zinazotoa huduma kwa wananchi. Ametoa onyo hilo jana (Jumapili, Desemba 21, 2025) wakati akizungumza na wagonjwa na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea hali halisi ya utoaji huduma siku za wikiendi katika hospitali hiyo. Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ratiba ya kukagua ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, mara baada ya kuwasili wilayani humo akitokea Ruangwa, aliamua kuanzia kwanza hospitalini kisha akaenda kwenye ukaguzi wa jengo hilo. Akiwa hospitalini hapo, alienda moja kwa moja kwenye chumba cha daktari wa zamu ili apate utaratibu wa kumhudumia mgonjwa pindi anapofika hospitalini na akaelezwa kwamba ni lazima mgonjwa aanzie mapokezi na kukata cheti ndipo aje kwa daktari. Hata hivyo, Waziri Mkuu alikuta wagonjwa wawil...
Marato tv - Sauti ya Jamii