Skip to main content

Posts

Showing posts from October 19, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhe.Deo Mwanyika(Mb) awahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura

Mbunge wa Njombe Mjini Mhe.Deo Mwanyika amewahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura , zoezi litakalohitimishwa Oktoba 20, 2024. Ameyasema hayo Oktoba 19, 2024 wakati akijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika Mtaa wa Uwemba. Amesisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi kwa kuchagua viongozi katika mitaa na vijiji. Ameongeza kuwa kujiandikisha ni muhimu lakini kushiriki kupiga kura ni muhimu zaidi  kwani mwananchi unakwenda  kuchagua kiongozi unayemtaka  kwa ajili ya maendeleo ya mitaa na vijiji vyetu.      *Serikali za mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze kushiriki uchaguzi*

Tanzania na Iran zasaini hati saba za makubaliano ili kukuza diplomasia ya uchumi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Iran zimesaini hati saba za makubaliano ili kukuza diplomasia ya uchumi baina ya mataifa hayo mawili. Hafla ya kusaini hati hizo za makubaliano imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Oktoba, 2024, katika mkutano wa tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Iran. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Kiislaam ya Iran, Mhe. Golamreza Nouri Ghezelcheh walishuhudia zoezi hilo la uwekaji saini hati hizo lililohusisha Wizara za Kisekta, baadhi ya Taasisi za Umma na Taasisi binafsi. Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliohusisha Viongozi wa ngazi za juu za Serikali za nchi hizo, wakiwemo Mawaziri, Mhe. Balozi Kombo amemshukuru Mhe. Golamreza Nouri kwa jitihada zake za kuimarisha ushirikiano wa uwili na azma yake katika kuongeza maeneo ya ushiriki...

Rais Samia Suluhu Hassan aipongeza yanga kwa ushindi dhidi ya simba

 Hongereni Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wenu wa Ligi Kuu. #KariakooDerby  Nawatakia nyote kheri katika michezo yenu inayofuata. Endeleeni kutupa burudani huku Taifa likiendelea kuchapa kazi kwa amani, umoja, utulivu na mshikamano.

Waziri Mavunde aeleza umuhimu wa madini bonanza

*Awahamasisha Watumishi kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa* *GST  Yazoa Medali za kutosha* *Madini Yanga Yanyakua Ubingwa* *Dodoma* Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameeleza kuhusu umuhimu wa Madini Bonanza na kueleza kuwa limelenga kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya  Watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kuifanya Wizara kuwa familia moja. Amesema hayo leo Oktoba 19, 2024 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin – Miyuji jijini Dodoma, wakati akizungumza katika Madini Bonanza lililowajumuisha Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake.  " Ninawapongeza kwa bonanza hili kwasababu linatusaidia kukaa  pamoja, kufurahi na kufahamiana zaidi," amesema. Aidha, amewasisitiza watumishi  kujenga utamaduni  wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao, na kuongeza," kama mnavyofahamu hivi sasa takwimu  zinaonesha kuna changamoto kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mazo...

Mama Mary Majaliwa ajiandikisha katika kitongoji cha Nanguriwe-Ruangwa

Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akijiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa na Vijiji,  utakaofanyika Novemba 27, 2024. Waziri Mkuu alijiandikisha kwenye kituo cha shule ya msingi Nandagala iliyopo kitongoji cha Nanguruwe, Kata ya Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi. Oktoba 19, 2024 Kushoto ni Afisa Uandikishaji Bw. Alexander Mmole