Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameendelea kuwezesha vijana mkopo nafuu wa pikipiki. Leo aprili 22,2025 vijana 75 wameingia kwenye utaratibu huo na kupata pikipiki ambazo watarejesha kwa kipindi cha miezi 11 na kuweza kumuliki. Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo mbunge huyo amesema lengo lake ni kusaidia vijana waweze kumiliki pikipiki zao na kuiiinua kiuchumi. Amesema amekubaliana na moja ya kampuni zinazouza pikipiki na kijana anayetoa kiasi cha shilingi laki 3 anamuongezea laki 1 na elfu 9 na kuendelea kulipa kidogo kidogo. Mathayo amesema mkopo huo ni nafuu tofauti na mikopo mingine ya gharama kubwa na inayolipwa kwa muda mrefu ambayo itawasaidia vijana. Mbunge huyo amesema hii ni awamu ya pili ya vijana kuwezeshwa kwenye upande wa pikipiki na kudai kuendelea na utaratibu huo kila vijana watapojitokeza. " Hii ni awamu ya pili tunawapatia vijana pikipiki za mkopo nafuu ili baadae waweze kuzimiliki na kufanya shughuli zao ...
Marato tv - Sauti ya Jamii