Skip to main content

Posts

Showing posts from July 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Trump asifu Rais wa Liberia kwa ufasaha wa Kiingereza

WASHINGTON, MAREKANI KATIKA tukio nadra sana, Rais wa Marekani Donald Trump amemsifia kiongozi wa Afrika kwa kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha. Trump mnamo Jumatano alikutana na kundi la marais kutoka Afrika ambao wanazungumza lugha mbalimbali. Walitumia nafasi hiyo kutoa wito wa kukuzwa kwa uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na nchi zao. Hata hivyo, kilichomteka makini Trump ni jinsi Rais wa Liberia Joseph Boakai alivyozungumza Kingereza kwa ufasaha akipigia debe kuimarishwa kwa uhusiano kati ya taifa lake na Marekani. “Liberia ni rafiki mkubwa wa Amerika na tunaamini katika sera yako ya kufanya Marekani iwe bora tena (MAGA),” akasema Rais Boakai kwenye Ikulu ya White House wakati wa mkutano huo wa uwekezaji na marais wa Guinea Bissau, Senegal, Mauritania, Gabon na Liberia. “Tunataka kukushukuru sana kwa nafasi hii tukizi ya kukutana nasi,” akaongeza. Trump alifurahishwa na ufasaha wa Boakai hata akauliza mahali ambapo kiongozi huyo alisomea lugha. “Kingereza kizuri na bora zaidi...

Vyakula vinavyosaidia kuimarisha afya ya mbegu za uzazi za kiume

AFYA ya manii huathiriwa na lishe, mtindo wa maisha, na afya kwa ujumla. Kuna baadhi ya vyakula vilivyothibitishwa kusaidia kuongeza ubora, wingi, kasi, na nguvu ya mbegu za kiume. Baadhi ya vyakula hivi muhimu ni pamoja na: Karanga na mbegu Kwa mfano, mbegu za mlozi, walnuts, mbegu za boga, chia, flax seeds. Vyakula hivi vina afya kama vile omega-3 fatty acids, madini ya zinki, na selenium — virutubisho vinavyosaidia kuimarisha mwendo, muundo, na uzalishaji wa manii. Samaki wenye mafuta Kwa mfano, samoni, sadini na samaki wa jamii ya bangala. Vyakula hivi vina kiwango kikubwa cha omega-3 ambacho husaidia kuboresha mtiririko wa damu kwenye viungo vya uzazi na kuongeza ubora wa mbegu. Mayai Mayai yana protini nyingi na virutubisho kama vitamin B12 ambavyo ni muhimu kwa utengenezaji mzuri wa manii. Mboga za majani ya kijani:Kwa mfano, spinachi na sukuma wiki. Mboga hizi zina viwango vya juu vya folate (vitamin B9), virutubishi ambavyo ni muhimu kwa afya ya kijeni ya manii. Matunda yenye ...

Besigye azindua chama kipya cha kisiasa akiwa korokoroni

  KAMPALA, UGANDA CHAMA cha People’s Front for Freedom (PFF) kimezinduliwa jijini Kampala huku kiongozi wake Kizza Besigye akiendelea kuzuiliwa gerezani kwa kosa la uhaini. Wakati wa shughuli hiyo, wafuasi walibeba picha ya Besigye iliyowekwa fremu huku wakimshabikia na kulaani utawala wa Rais Yoweri Museveni kwa kumdhulumu mwanasiasa huyo “bila sababu maalum”. Kiongozi huyo wa upinzani, alitarajiwa kuhudhuria hafla hiyo aidha kwa njia ya video au kwa kutuma taarifa isomwe kwa wafuasi wake. Bw Besigye, ambaye amewania urais kwa mara ya nne, amekuwa kizuizini tangu Novemba mwaka jana alipokamatwa Kenya na kushtakiwa kwa kupanga njama ya kumwondoa mamlakani Rais Museveni. Waendesha mashtaka wanadai kiongozi huyo wa upinzani alikuwa akisaka usaidizi wa kijeshi kutoka mataifa ya nje ili kuhujumu Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF). Lakini mawakili na wafuasi wa Besigye wanadai mashtaka hayo yamechochewa kisiasa kwa lengo la kumzuia kuwania urais dhidi ya Museveni, 80, katika uchaguzi mkuu...

Katibu Mkuu Maswi Aipongeza Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Usimamizi wa Mashauri

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imepongezwa kwa kuendelea kusimamia kwa weledi mashauri ya madai na usuluhishi hatua ambayo imesaidia Serikali kuongeza kasi katika kuwaletea wananchi maendeleo. Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ndugu Eliakim Maswi alipotembelea banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya 49 ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. Ndugu Maswi alisema kuwa uwepo wa weledi na ufanisi katika uendeshaji wa mashauri ya madai, usuluhishi, Katiba, Haki za Binadamu na Uchaguzi katika Ofisi hiyo umeongeza kasi katika kupunguza na kutatua migogoro ya kisheria kwa njia ya majadiliano badala ya kutumia muda mrefu kusikiliza shauri hilo mahakama ni.  Ameongeza kuwa fedha zinazookolewa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali zimekuwa zikitumika kujenga miradi mikubwa ya maendeleo ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kuwarahisishia wananchi kote nchini katika kufanya shughuli zao za kujiletea maende...

Ruto apewa fursa ya kuajiri makamishna wa IEBC kihalali

 MAHAKAMA Kuu Nchini Kenya imekosoa hatua ya Rais William Ruto kuajiri makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mpaka(IEBC)bila idhini yake ikisema agizo la mahakama lililokuwepo lilistahili kuheshimiwa. Hata hivyo, korti hiyo ya Milimani wakati huo huo imetupa kesi iliyotaka uteuzi mzima wa Makamishna hao ufutwe, jambo linalotoa nafasi kwa Rais kuwaajiri kihalali. Majaji Roseline Aburili, John Chigiti na Bahati Mwamuye walimkosoa vikali Bw Ruto kwa kuajiri Erastus Ethekon Edung na wenzake wakati ambapo kulikuwa na agizo la mahakama la kusitisha zoezi hilo hadi kesi iliyowasilishwa mahakamani isikizwe na kuamuliwa. Majaji hao hata hivyo walisema hawakupata ithibati yoyote kwamba uteuzi mzima umekiuka katiba na Kwamba madai ya walalamishi kwamba uteuzi haukufikisha vigezo vya usawa wa kimaeneo hayakuwa na mashiko na kwamba malilio walalamishi waliyotaka hayakuwiana na madai waliyowasilisha. Aidha Mahakama hiyo imemkosoa Dkt Ruto kwa kupuuza agizo lamahakama, korti hiyo ilisema m...

Tanzania ina Umeme wa Kutosha – Dkt. Biteko

📌 Asema ni jitihada za uwekezaji uliofanywa na Rais Dkt. Samia 📌 Aipongeza TANESCO kwa kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania ina umeme wa kutosha hatua ambayo imechangiwa na kukamilika kwa  Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme ukiwemo Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ambao pekee unazalisha Megawati 2115. Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo Julai 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia katika vituo vya  Kinyerezi I, Kinyerezi I Extension na Kinyerezi II ambapo amesema licha ya kazi kubwa inayofanywa na TANESCO yapo baadhi ya maeneo yalikua na changamoto ya upatikanaji wa umeme lakini mpaka sasa yameendelea kuimarika. Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko amefafanua kuwa ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme unaendana na mahitaji ya ongezeko la watu TANESCO inatarajia kuongeza uzalisha...